13 Mar 2018

Aliyejiuzulu Bavicha: Mimi Bado Mwanasiasa

Aliyejiuzulu Bavicha: Mimi Bado Mwanasiasa
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Gertrude Ndibalema amesema licha ya kujiuzulu wadhifa huo, hana mpango wa kuachana na siasa.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Machi 13, 2018  amesema siasa ni maisha na ni ngumu kwake kama kijana kuachana nayo, “nisiposikika katika ulingo huo wa siasa nitaonekana tu. Siwezi kufanya uamuzi wa ajabu kama huo wa kuacha siasa, nimejiuzulu nafasi hiyo, lakini mimi bado ni mwanasiasa ukizingatia umri unaniruhusu.”

Amesema katika nafasi ya uongozi aliyokuwa nayo changamoto zilikuwa nyingi, lakini alikuwa anatoa ushauri kwa viongozi wa chama na kwamba zipo zilizofanyiwa kazi na ambazo hazijafanyiwa kazi.

Kuhusu demokrasia nchini amesema, “Nchi ili iwe na  demokrasia lazima iwe na siasa safi na uongozi bora, swali la kujiuliza ni kwamba Tanzania kuna vitu hivyo viwili.”

“Kama hakuna vitu hivyo ina maana bado hatuna demokrasia, kuna kukatazwa mikutano ya siasa, kukatazwa maandamano, kuna vitu vichache vikifanyiwa kazi kila kitu kitakuwa sawa.”

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 alitangaza kujiuzulu Machi 12, 2018 kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsiBonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger