Amber Rose Atokwa Povu Kisa Mwanaye

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Amber Rose Atokwa Povu Kisa Mwanaye


MWANAMUZIKI Amber Rose, amejikuta akitokwa povu la kutosha baada ya njemba mmoja kumkashifu mwanaye mwenye umri wa miaka mitano, Sebastian kupitia Mtandao wa Kijamii wa Twitter, kwamba anatabia za kishoga.



Kashfa hizo kwa Sebastian ambaye Amber Rose amemzaa pamoja na rapa Wiz Khalifa, zilifuata baada ya Amber Rose kutupia mtandaoni video ikimuonesha Sebastian akifungua zawadi na kumkabidhi mwanamuziki Taylor Swift, ambapo katika zawadi hiyo kulikuwa na tiketi mbili kwa ajili ya ziara za kimuziki anazotarajia kufanya Taylor.



Njemba huyo aliandika hivi;“Ukimuangalia mtoto huyo,anavyoongea, anavyotenda lazima utaelewa tu hawezi kuwa mwanaume sawa!”Baada ya komenti hiyo baadaye Amber naye alijibu mapigo kwa kusema; “Huwezi kusema motto wa miaka mitano anajihusisha na ushoga. Hata hivyo mtoto wangu si wa jamii, atabaki kuwa wangu na lazima maneno mengi yasemwe kwa sababu ni wa kipekee zaidi.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad