Ben Pol Kumuoa Ebitoke ?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ben Pol kumuoa Ebitoke ?Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye inasemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, amewataka watu kuwa na subira juu ya kujua ukweli uliyopo baina yao kwa madai hakuna jambo linaloweza kufichika milele.


Ben Pol ametoa kauli hiyo baada ya kila kukicha kusumbuliwa na waandishi pamoja na mashabiki zake kiujumla kutaka kujua ukweli juu ya ukaribu wake na mchekeshaji huyo ambaye yeye binafsi anatangaza kuwa yupo kimapenzi na Ben kimapenzi kila aulizwapo na watu.

"Sijawahi kutoka katika mahusiano na Ebitoke yaani kila kitu kipo vile vile hakuna kilichobadilika baina yetu. Siwezi kusema kama nipo kwenye mahusiano naye ila tupo karibu sana", amesema Ben Pol.

Pamoja na hayo, Ben Pol ameendelea kwa kusema "watu wawe wanasubira maana wanauliza sana juu ya hilo lakini mimi ninachoweza kusema watu wawe na subira kila kitu kitakuja kuwa bayana kwasababu hakuna kitu kinachowez kuwa siri milele au kukwepeka kila siku. Wanachotaka kukiona watu watakiona tu wenyewe kwa macho yao kwa hiyo wasiwe na haraka kiasi hicho".

Kwa upande mwingine, Ben Pol jana kupitia EATV ameweza kutambulisha rasmi video ya wimbo wake mpya inayojulikana kwa jina la 'natuliza boli' ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri katika mtandao wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad