Davina Akubwa na Kashfa ya Utapeli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Davina Akubwa na Kashfa ya Utapeli
STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amejikuta anaingia kwenye kashfa ya utapeli baada ya mtu ambaye hajafahamika kutumia jina lake kutapeli watu kupitia Mtandao wa Facebook.

Akiongea na Risasi Jumamosi, Davina alisema hakuna kitu kinachomnyima raha kama mtu kutumia jina lake kwa mambo ya kitapeli kwani watu wasiojua wanamchukia wakidhani ni yeye, kitu ambacho hajawahi kufanya hata siku moja.


“Kitendo cha mtu huyo kutumia jina langu halafu anaomba hela kwa watu kinanisikitisha na kunitia doa kwani tabia hiyo mimi sijawahi kuifanya, nawaomba watu wawe makini katika hilo maana huyo ni tapeli mkubwa anayetumia vibaya majina ya mastaa,” alisema Davina.

Baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakitumia majina ya mastaa kutapeli watu mitandaoni na hata Jackline Wolper aliwahi kukutwa na janga hilo hivi karibuni.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad