Familia ya Diamond Yacharuka Mbaya Baada ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Familia ya Diamond Yacharuka Mbaya Baada ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani
Siku chache baada ya Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuonekana akiwapeleka watoto wake kanisani, imeelezwa kuwa, familia ya mzazi mwenzake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imecharuka vibaya kwani haifurahishwi na kitendo hicho baada ya kuachana kwao.



Taarifa za kuaminika ambazo Amani ilizipata kutoka ndani ya familia ya Diamond zilidai kuwa, awali waliona ni jambo la kawaida lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, wanaona ni tatizo.

“Awali Zari alipotupia picha ya kwanza ikionesha ameenda kanisani na watoto, tuliona labda ni maombi ya mara moja na pengine haiwezi kuwa tatizo lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, tunaona amekomaa na kanisani sasa tunaona kama inaweza kuja kuwa tatizo hapo baadaye na watoto wakawa njia panda.



“Si unajua wale watoto ni waislamu kwa sababu siku zote watoto huwa wanafuata kwa baba, sasa baadaye watakaporudi kwa Diamond na wakawa wameshazoea kwenda kanisani itakuwaje?” alihoji Amani mmoja wa wanafamilia aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.


Diamond na familia yake.



MAMA, BABA DIAMOND HAWAKUFURAHISHWA

Taarifa hizo za ndani ya familia zilizidi kueleza kuwa, mama na baba Diamond wote hawakufurahishwa na jambo hilo japo Diamond mwenyewe hakuonekana kulimaindi sana.

“Mama na baba Diamond ndiyo wamecharuka sana japo Diamond anaonekana kutomaindi kivile.

“Unajua wazazi bwana wenyewe wanaona kuwaacha watoto wafuate kwa mama si sawa na ndiyo maana wamekuja juu, wanamtaka Diamond asimame kama mwanaume,” taarifa za ndani ya familia zilidai.



TAARIFA ZAIDI

Taarifa zaidi zilieleza kuwa, tayari baadhi ya ndugu wameshaanza kuweka vikao vya siri ili ikiwezekana wamweke kiti moto Diamond ili aweze kumvaa mzazi mwenziye haraka ili awe pia anawapeleka watoto madrasa.

“Unajua bora tungekuwa tunaona hata siku mojamoja anawapeleka madrasa angalau tungeona ni sawa lakini sasa hivi yeye kila siku ni kanisani tu,” alisema mmoja wa wanafamilia.



WATAJA SIRI ZARI KUUPENDA UKRISTO

Aidha, wanafamilia hao wamedaiwa kuwa na hofu zaidi ya Zari kuwabatiza watoto hao kwani historia inaonesha mrembo huyo alikuwa mkristo mzuri baada ya kuolewa na marehemu mumewe, Ivan Ssemwanga hivyo huenda ndiyo sababu ya kufanya maamuzi hayo.

“Unajua Zari alibobea kwenye ukristo na inaonekana anaipenda sana dini hiyo kuliko ya baba watoto wake sasa kama amerejea huko, ni rahisi sana kuwabatiza watoto wa Diamond,” alisema mwanafamilia mwingine.


Tiffah na Nillan.



MAMA DIAMOND ATAFUTWA

Amani lilimvutia waya mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje suala hilo lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

Alipotafutwa baba Diamond, Abdul Juma aliweka wazi kuwa kama familia hawajafurahishwa na kitendo cha Zari kuwafundisha kuhusu mafundisho ya Kikristo pekee.

“Hatukatai dini ni dini tu lakini kilichotushtua ni kwa nini tunaona anawapeleka upande mmoja tu.



“Unajua hata kama yeye ameamua kurudi kwenye Ukristo lakini watoto anapaswa kuzungumza na mwenzake ili waamue pamoja,” alisema baba Diamond.

Baba Diamond alimalizia kwa kutoa msimamo mkali kuwa, kama familia watamsisitiza Diamond azungumze na mzazi mwenzake na waangalie uwezekano wa kuwapeleka watoto hao madrasa ili pia waifahamu dini ya baba yao.


Mzee Abdul.



DIAMOND HAPATIKANI

Alipotafutwa Diamond wakati tunakwenda mitamboni juzi, kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana. Hata hivyo, ilibainika kuwa wakati huo staa huyo alikuwa nje ya nchi kwa shughuli za kimuziki.



TUMEFIKAJE HAPA?

Hivi karibuni, Zari alitangaza kummwaga Diamond kufuatia staa huyo kudaiwa kumsaliti mara kwa mara na habari zake kusambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Baada ya kuachana, watoto wawili waliofanikiwa kuzaa walipokuwa pamoja, wanaishi na Zari nchini Afrika Kusini huku Diamond akiendeleza maisha yake Bongo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona dai huwa anavaa misalaba?

    ReplyDelete
  2. Huyo daimond mwenyewe ni mUislam jina tu, ndio maana wala 'haja'mind' watoto wake kupelekwa kanisani.....MAMBO-YA-NGOSWE-MUACHIE-NGOSWE-MWENYEWE

    ReplyDelete

Top Post Ad