FBI Aliyetambua Shambulio la Osama Bin Laden Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

FBI Aliyetambua Shambulio la Osama Bin Laden Afariki Dunia
SHIRIKA la Uchunguzi la Marekani (FBI) limesema limempoteza mwanamama mmoja ambaye ni miongoni mwa waliotambua shambilizi la kigaidi la Septemba 11, 2001 lililofanywa na Osama BinLaden, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.




Melissa S. Morrow alifariki juzi Alhamisi akiwa na miaka 48 kwa kansa ya ubongo huku ikielezwa kuwa, huenda kifo chake kilisababishwa na kuwekewa vitu vyenye sumu (kemikali).

Mtaalam huyo wa uchunguzi, amefanya kazi ndani ya FBI kwa miaka 22, na wakati umauti unamfika alikuwa ana siku chache tangu ahamishiwe katika kituo kipya cha kazi, Kansas City.




Taarifa ya FBI imeeleza kuwa, Morrow alikuwa amejitoa kwa kiasi kikubwa kulitumikia taifa lake kwa kuchunguza na kubaini ukweli wa shambulio la Spetemba 11, katika Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon,.

Inadaiwa mama huyo baadaye alikutwa kwenye  ghala lenye sumu mwaka 2013 jambo lilliloplekea kuzorota wa kwa fya yake  licha ya kutibiwa kwa zaidi ya wiki 10 huku akikusanya taarifa kuhusu shambuilio hilo lililotikisa dunia.


Morrow alijiunga na FBI mwaka 1995 na mazishi yake yatafanyika Country Club Christian Church eneo la Kansas City, Jumanne mchana.

Msiba huo umetokea ikiwa ni wiki moja tu tangu kifo cha aliyekuwa kapteni kwenye kikosi cha uokoaji, Thomas Phelan aliyewaokoa waathirika wa shambulio la September 11 ambaye naye amefariki kwa Kansa akiwa na miaka 45 huko Lower Manhattan.



Thomas Phelan, March 16  ambapo naye anadaiwa kifo chake kimesababishwa na kuwekewa mvuke wa sumu huko Ground Zero.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad