Hivi Ndivyo Daimond, Dogo Janja Wanavyowatesa Mama Wema , Mama Irene Uwoya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hivi Ndivyo Daimond, Dogo Janja Wanavyowatesa Mama Wema , Mama Irene UwoyaNDOA au uhusiano wa mapenzi bila shaka ni jambo la kheri ambalo kila mmoja wetu hupenda watu wanaomzunguka kufurahia chaguo lake na kumpa Baraka anazostahili.



Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wengi, lakini tofauti kwa mastaa wa fi lamu Irene Uwoya pamoja na Wema Sepetu, ambao uhusiano wao umekuwa ni jambo lisilokubalika kwa wazazi wao kwa msemo rahisi unaweza kusema paka na panya, huku wakiamini kwamba wapenzi walionao hawawastahili.


Kwa upande wa wawili hawa zilianza kama tetesi kwamba wanatoka kimapenzi lakini baadaye wakaibuka na ndoa kabisa na kuhalalisha tetesi za ‘kumegana’ kisela.Hata hivyo toka wadai kufunga ndoa, kwa upande wa mama mzazi wa Uwoya, ameonekana dhahiri hamkubali hata kidogo Dogo Janja.

Mara kwa mara akihojiwa na waandishi wa habari amekuwa akikanusha juu ya kuitambua ndoa hiyo na kusema mwanaye hajafunga ndoa kwani hajahusishwa pamoja na maneno mengine ya kumponda Dogo Janja.Ambapo kutokana na maneno hayo inawezekana


Wema akiwa na Mama yake

kabisa hata akiwa anasali, mama Uwoya pengine huomba Mbongo Fleva huyo amuache mwanaye.Lakini kwa Uwoya inaonekana hasikii wala haambiliki. Kwa upande wa mahaba, kwa Dogo Janja ndiyo amefi ka Kigoma mwishowa reli na kama kuongea, ameamua kumuacha mama yake azungumze tu lakini anasonga mbele.



WEMA SASA NA DIAMOND!

Kama ilivyo kwa mama yake Uwoya,kwa upande wa mama Wema ndiyo hataki kabisa kumsikia Diamond. Si mara moja wala mbili mama Wema kuibuka na kuanza laivu Diamond,kwamba hamfai mwanaye na si mtu sahihi, wakati mwingine amekuwa mpaka akimkashifu kwa kumuita ‘domo’ japokuwa Wema mwenyewe amekuwa akiingia naye kwenye uhusiano na kutoka



Sasa pamoja na hayo jiulize Wema breki zinakaba kwa Diamond? Jibu ni kwamba hapana!Maana ingekuwa hivyo Wema angekuwa mbali na Diamond kimahaba, kwani tetesi mpya mjini kwa sasa ni kwamba wawili hawa wanatoka tena kimapenzi baada ya kumwagana kipindi cha nyuma.



Sasa ili watu hawa wanne wapate furaha na Baraka kutoka kwa wazazi wao ninashauri ni muhimu kutazama pia suala hili kwamaelewano kati ya wapenzi wao na mama zao.Ikiwezekana hata kukaa chini na wazazi wao na kuzungumza juu ya maisha yao ya uhusiano maana katika suala la kupenda kila mtu ana uhuru wa kupenda na kupendwa.



Kama ni machaguo yao sahihi na wakizungumza vyema na wazazi wao bila shaka atawaelewa na kuwapendapia. Zaidi watawapa baraka katika uhusiano huo na kuwatakia kheli kwani raha ya uhusiano ni watu wenu wakaribu kufurahia uhusiano huo na kuishi nanyi vizuri.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad