Mwigulu Awataka Walimu Kutumia Fimbo Kutoa Maadili kwa Wanafunzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwigulu Awataka Walimu Kutumia Fimbo Kutoa Maadili kwa Wanafunzi

Waziri wa Mambo ya ndani, Dk  Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.


Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari  Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida,  Dk Nchemba amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.

"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini kuna watu wengine hawaoni haya ila wao ni kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," amesema Dk Mwigulu.

Amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.

Mbali na hayo Dk. Nchemba ameongeza kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.

"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad