Kombe la Dunia Lamaliza ‘Bifu’ la Diamond, Nahreel

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kombe la Dunia Lamaliza ‘Bifu’ la Diamond, Nahreel
Chumba cha habari Dar. Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitatimua vumbi nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu  zimewakutanisha mahasimu wawili, Diamond Platnumz na mtayarishaji Nahreel waliotofautiana baada ya kufanya kazi pamoja miaka mitatu iliyopita.

Daimond alitofautiana na Nahreel baada ya kuondoa utambulisho wa mtayarishaji huyo katika wimbo Nana aliomshirikisha Mr Flavour wa Nigeria.

Nahreel aliyetengeneza wimbo huo alikasirishwa na kitendo cha Diamond kuondoa utambulisho wake maarufu “Nahreel on the beat” katika video.

Ilichukua muda mrefu mashabiki kujua mtayarishaji wa wimbo huo kabla ya Nahreel kulalamikia hatua ya utambulisho wake kuondolewa na ndipo Diamond alipojitokeza kujitetea kwamba hakufanya hivyo kwa makusudi.

Katika utetezi wake alisema Nahreel alimpa wimbo ambao hauna utambulisho, hivyo baada ya kumaliza kurekodi video ilishindikana kuweka kipande kingine na kwamba hakufanya makusudi.

Hata hivyo, Coca Cola nchini imewakutanisha tena kutengeneza kipande cha wimbo Colors maalumu kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia.

Kipande cha Diamond kilichounganishwa na wimbo huo kimetengenezwa na Nahreel ambao kwa mara ya kwanza uliimbwa na mwanamuziki wa Marekani, Jason Derulo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad