Waziri Mkuu Aitaja Mikoa Minne Inayoongoza kwa Utoro wa Wanafunzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu Aitaja Mikoa Minne Inayoongoza kwa Utoro wa Wanafunzi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaja mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari.

Waziri mkuu pia ameitaja mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.

Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa ameitaja mikoa hiyo leo Jumatatu Aprili 2,2018 akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani Geita.

Mbio za Mwenge zitakazohitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga zinaongozwa na kauli mbiu “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu.”

Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1) na Shinyanga (asilimia 6.3).

Kwa shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita (asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu (asilimia 2).

“Kwa jumla utoro wa wanafunzi wa sekondari ni mkubwa kuliko shule za msingi. Naikumbusha mikoa yote niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwamo wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa kutumia utaratibu wa sheria zilizowekwa,” amesema Majaliwa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad