'CCM Imedhulumiwa Sana' - Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

'CCM Imedhulumiwa Sana' - Rais Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli, amesema kwamba mali za Chama hicho zimeibiwa kwa kiasi kikubwa  kutokana na usimamizi mbovu ulikuwa unafanywa na watendaji wa chama hicho.


Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 21, 2018 katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba Jijini Dar es salaam baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya kuhakiki mali za CCM nchi nzima na kuongeza kuwa haiwezekani Serikali inapambanua na ufisadi wakati chama tawala hakioneshi mfano kupinga ubadhirifu.

“Ripoti imesheheni mambo mengi, CCM imedhulumiwa kweli, inaumiza sana mpaka nimechoka, lakini ndiyo hivyo nimeipokea lengo ni kuhakikisha tunakuwa na chama ambacho matumizi ya fedha na miradi inayosimamiwa na chama iwe miradi ya ukweli na isiwe ya utapeli” amesema Rais Magufuli

Rais Dkt. Magufuli ameongeza kwamba ripoti hiyo ataiwasilisha kwa wajumbe wa mkutano wa Halmashuri kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) ili kuijadili ripoti hiyo na badae kutoa maamuzi kutokana na malekezo ya wajumbe hao.

Disemba 20, 2017 katika kikao cha Halmashauri kuu CCM (NEC) Rais John Magufuli aliunda tume ya wajumbe tisa wakiongozwa na mwenyekiti Dkt. Bashiru Ali Kakurwa ambapo tume hiyo ilipewa jukumu la kuhakiki mali za Chama nchi nzima kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad