Gigy Money, Amber Lulu ni Mavideo Queen Ambao Hawana Mvuto Kabisa- Kim Nana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gigy Money, Amber Lulu ni Mavideo Queen Ambao Hawana Mvuto Kabisa- Kim Nana
MWANADADA mwenye mvuto wa pekee kwenye video za Kibongo, Lilian Paul Kessy ‘Kim Nana’ ambaye ameuza sura kwenye video nyingi za Kibongo zikiwemo za mwanamuziki Becka Flavour amefunguka kwamba, hakuna ma-video queen ambao hawakubali kama Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Lulu Eugen ‘Amber Lulu’. Msikie akihojiwa na Showbiz Xtra;

Showbiz Xtra: Kwa nini huwakubali Gigy na Amber?

Kim: Sijui tu, naona hawanivutii kabisa na hawana mvuto wa kuwa ma-video queen. Bora ‘wa-stick’ hukohuko kwenye muziki walikokimbilia.

Showbiz Xtra: Kibongobongo kwa sasa ni video queen gani unamkubali?

Kim: Bongo hayupo zaidi ya mimi mwenyewe.

Showbiz Xtra: Unaamini wewe ndiye zaidi ya wote?


Kim: Ndiyo.

Showbiz Xtra: Kwani unachukua kiasi gani kwenye video moja?

Kim: Kwa namna ‘nilivyoji-brand’ kwa sasa, sichukui chini ya laki tano.

Showbiz Xtra: Sasa laki tano huoni wewe ndiye upo chini, wenzio wanachukua hadi mamilioni!

Kim: Mh! Msanii gani anatoa mamilioni kwa sababu ya video? Ukisikia mtu anasema hivyo ni uongo, hao wasanii wakubwa wenyewe wanapenda wadada wazuri kama mimi tuuze sura bure kwenye video zao. Hakuna anayechukua milioni kwenye video.

Showbiz Xtra: Kwa hiyo kutokana na mkwanja mdogo mnaolipwa kwenye video ndiyo maana wengi wanajiuza?

Kim: Siwezi kuwazungumzia wengine. Lakini kwa upande wangu sijiuzi na ninajishughulisha kusimamisha mambo yangu. Nina ‘brands’ za vitu vyangu nimeachia hivi karibuni ambavyo ni tisheti, lipstiki na ninategemea baadaye kuja na sabuni pamoja na vitu vingine vingi.

Showbiz Xtra: ‘All the best’ lakini inasemekana pia wanamuziki wanaowapa dili kwenye video zao huwa ‘wanawatafuna bila huruma’?

Kim: Ha! Ha! Haa! Si kweli, mimi hiyo haijawahi kunitokea ‘nikatafunwa bila huruma’, labda ma-video queen wengine. Mimi ninajiheshimu, nikiitwa na mwanamuziki kuhusu kazi, tunafanya halafu basi. Tutaendelea kuwasiliana kwenye mambo mengine, lakini siyo mapenzi. Sijawahi kutoka kimapenzi na staa yeyote Bongo na sitarajii hilo kwa sababu kuwa na uhusiano na mastaa kuna-umiza kichwa. Wengi hawa-jatulia.

Showbiz Xtra: Nini hasa ‘future’ yako kwenye masuala ya kuuza sura katika video?

Kim: Kukuza jina zaidi na kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama Diamond, Ally Kiba na Jux.

Showbiz Xtra: Shukrani sana kwa ushirikiano wako.

Kim: Pamoja sana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad