Breaking News: Katibu Itikadi CCM Mkoa wa Simiyu Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Danhi Makanga,  amefariki dunia leo Jumapili Juni 24, 2018 wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza katika ajali iliyohusisha pikipiki na Bajaj.

Taarifa za kifo cha Makanga ambaye amewahi kuwa mkuu wa wilaya na mbunge zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.

Sweda amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi eneo la Nyashishi na kwamba marehemu alikuwa amepanda pikipiki iliyogongana na Bajaj na kusababisha kifo chake na dereva wa pikipiki hiyo.

“Ni kweli ajali imetokea na wote wawili wamefariki ila dereva wa Bajaj amepata majeraha. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, “amesema Sweda.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad