Mmiliki wa Mgahawa wa Bunge Akamatwa na Samaki Haramu...... Apigwa Faini Baada ya Kukiri Kosa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mmiliki wa Mgahawa wa Bunge Akamatwa na Samaki Haramu...... Apigwa Faini Baada ya Kukiri Kosa
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi, imekamata samaki aina ya sato (wasiofikia kiwango cha kuvuliwa) kiasi cha kilo mbili kati ya 100 waliokuwa wakiuzwa kinyume cha sheria katika mgahawa wa ofisi ya Bunge jijini Dodoma leo JUmanne, Juni 19, 2018.



Kufuatia tukio hilo, mmiliki wa mgahawa huo, Daniel Lamba, amepigwa faini ya Sh. 300,000 baada ya kukiri kosa la kukutwa na samaki hao wachanga.

Kaimu Meneja wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu wa wizara hiyo, John Komakoma amesema samaki hao ni ambao hawapaswi kuvuliwa kwa mujibu wa kisheria.

“Hawa samaki tumewakamata kwa kuvuliwa kinyume cha sheria, mmiliki wa mgahawa huu amekiri kosa mwenyewe hivyo tumemtoza TSh. 300,000 ambayo atakwenda kulipia benki,” alisema Komakoma.



John Mpepele ambaye ni Msemaji wa wizara hiyo amesema aliyewapa taarifa za kuwepo samaki hao ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyekuja kwenye mgahawa huo jana asubuhi. “Waziri Mpina alipowaona samaki hawa, aliwatilia shaka na kutuagiza kuja kufuatilia,” alisema.



Aidha, mmiliki wa mgahawa huo, Bwana Daniel Labiaramba akikiri kosa kosa amesema; “Nakiri kosa ni weli, lakini katika kilo 100 nilizouziwa, ni ngumu sana kujua iwapo umewekewa samaki hawa, sikufanya hivi makusudi, kwani sikujua,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad