Msongo wa Mawazo Wamtemsa Freeman Mbowe, Azungumzia Hali yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


NA FATUMA MUNA
Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili imeimarika na ameruhusiwa kutoka hospitali huku akieleza kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni msongo wa mawazo na uchovu kupita kiasi.


Mbowe ambaye ni Munge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa CHADEMA ameweka hayo wazi wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari waliofika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo Jijini Dar es salaam.

Mbowe amesema afya yake ni nzima hadi sasa, baada ya kumaliza msiba ataendelea kufanya vipimo  maalumu vya kiafya kwa kadiri ambavyo atatakiwa na madaktari wake kama itakuwa ndani au nje ya nchi.

Mbowe pia amewashukuru viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na watanzania ambao walimtembelea na hata waliokuwa wakimuombea kwa njia mbalimbali katika kipindi hiki yeye na familia yake ikiwa na wale ambao walizuiwa kumuona kutokana na sheria za kitabibu

EATV
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad