Wema Sepetu Aanza Kujitetea Mahakamani Kesi Yake ya Dawa za Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wema Sepetu Aanza Kujitetea Mahakamani Kesi Yake ya Dawa za Kulevya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeaza kusikiliza utetezi wa mshtakiwa ambaye ni muigizaji, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abass,  baada ya mahakama hiyo kuwaona wana kesi ya kujibu katika mashtaka yanayowakabili ya kutumia dawa za kulevya.



Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.



Watuhumiwa hao wameanza kujitetea mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na washtakiwa hao wanatetewa na wakili Alberto Msando ambaye alikuwa akiwaongoza katika kuwauliza maswali juu ya nini wanafahamu kuhusiana na tukio hilo kuanzia Februari 4, 2017 hadi walipofikishwa polisi.



Kwa nyakati tofauti watuhumiwa hao wameeleza kila kitu wanachokifahamu juu ya tukio hilo ambapo hakimu Simba alikuwa akiandika kile walichokuwa wakieleza.



Kwa upande wa mashtaka, umeongozwa na wakili wa Serikali, Constantine Kakula, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 16 mwaka huu ambapo hakimu atatoa uamuzi.



Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad