5/21/2022

Bahari yameza Wahamiaji , Maelfu wako Njiani

 


Wahamiaji watatu wamethibitishwa kufariki na wengine kumi hawajulikani walipo, huku 40 kati yao wakiokolewa baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Pwani ya Mashariki ya Kati, Tunisia.


Boti hiyo iliyoondoka Pwani ya Sfax ikiwa na zaidi ya wahamiaji 50 raia wa Tunisia,  ilizama katika Mji wa Bandari katika jaribio la wahamiaji hao la kuingia Ulaya kinyime na sheria.


Msemaji wa Walinzi wa Kitaifa wa Tunisia, Houcem Jebabli  amesema Mji wa Sfax ni mojawapo ya sehemu kuu za kuondoka kwa wahamiaji wa Tunisia na wa kigeni kutoka maeneo mengi ya Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Pwani ya Italia.


“Na kasi ya kuondoka kinyume cha sheria huenda ikaongezeka msimu wa kiangazi unapokaribia maana majira haya hutumika sana na wahamiaji haramu,” amefafanua Jebabli.


Mwanzoni mwa Mei 2022, Serikali nchini Tunisia ilitangaza kupatikana kwa miili 24 ya wahamiaji baada ya boti zao kuzama kwenye ufuo huo wa Sfax.


Vilevile, kati ya tarehe 22 na 30 Aprili 2022, boti nne zilizama katika ufuo wa Sfax na kusababisha kuzama kwa wahamiaji 97 ambao waliokolewa, kupatiwa matibabu na kupona siku zilizofuata.Mwaka huohuo, wahamiaji wengine 15,671 wakiwemo wanawake 584 walifanikiwa kufika ardhi ya Italia kutoka Pwani ya Tunisia ikilinganishwa na wale 12,883 kati yao wanawake wakiwa 353 kwa mwaka 2020.


“Kiujumla zaidi ya wahamiaji 123,000 walitua Italia mwaka 2021 ikilinganishwa na wahamiaji 95,000 kwa mwaka 2020 ameongeza Jebabli.


Italia ni moja wapo ya sehemu kuu za kuingia Ulaya kwa wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini ambao wanawasili hasa kutoka Tunisia na Libya, nchi mbili ambazo zinaongoza kwa kiasi kikubwa cha wananchi wake kuikimbia tangu mwaka 2021

Manara na Barbara Watinga TFF, Wahojiwa na Kamati ya MaadiliMKURUGENZI wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez na Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara leo wametinga katika Ofisi za TFF ambapo waliiitwa kwa aili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya TFF.

Baada ya kutoka kuhojiwa na Kamati ya Maadili, CEO Barbara alisema kwa sasa hawezi kuongea chochote kwani wenye mamlaka ya kutoa tamko ni TFF.

Naye Haji Manara kwa upande wake alisema wamekatazwa kuongea chochote hivyo hawezi kusema chochote na amesisitiza hakuna ugomvi kati yao.

Barbara aliandikiwa barua ya kufika leo katika Ofisi za TFF akiwa na tuhuma ya kufanya mahojiano na Chombo cha Habari cha nchini Afrika Kusini cha Metro na kutamka baadhi ya maneno ambayo yanasemekana kuwa na ukakasi wa kuichafua Nchi, Klabu ya Yanga pamoja na Mpira wa Miguu wa Tanzania kwa ujumla.


Msemaji wa Yanga Haji Manara akiwa katika Ofisi za TFF
Kwa upande wake Haji Manara sababu ya wito wake haijawekwa wazi hadi sasa ingawa ni kweli kwamba wote wametinga katika Ofisi za TFF na tayari wamehojiwa na kamati ya Maadili ya TFF.

Kinachosubiriwa ni kuona je Kamati ya Maadili ya TFF itatoa uamuzi gani juu ya masuala waliyowaitia CEO Barbara pamoja na Msemaji wa Yanga Haji Manara

James Mbatia: Mimi bado mwenyekiti wa NCCR- MageuziMWENYEKITI    wa NCCR- Mageuzi, James Francis Mbatia, amedai kuwa unaoitwa, “mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama chake” uliomsimamisha wadhifa wake, “ni batili.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Hakuna mkutano wowote wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi, uliyoitishwa na uongozi wa chama. Kamati Kuu (CC), haijawahi kuitisha mkutano na hivyo, kinachoitwa mkutano wa NEC, ni kitu ambacho siyo halali,” ameeleza Mbatia.

Amesema, atashangaa ikiwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, atabariki maazimio ya mkutano huo.

Amesema, jana chama chake kilipeleka kwa msajili muhtasari wa kikao cha Kamati Kuu, ambapo pamoja na mengine, kumjulisha kusogezwa mbele kwa Mkutano wa Kamati Kuu na kumsimamisha kazi, Katibu Mkuu, Matha Chiumba.


 

Hata hivyo, Mbatia hakueleza MwanaHALISI anachukua hatua gani, kukabiliana na “mapinduzi hayo.”

Badala yake, mwanasiasa huyo aliishia kusema, “bado naendelea kujadiliana na wenzangu, kuona hatua za kuchukua.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kamati Kuu, iliyokutana mwishoni mwa wiki, iliamua kuusogeza mbele mkutano huo hadi 18 Agosti mwaka huu.

Lakini muda mfupi baadaye, Edward Simbeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma, ametoa taarifa kuwa Mbatia na baadhi ya viongozi wenzake, watakutana kujadili hatma ya chama chao, saa nane mchana wa leo Jumamosi.

Mkutano wa NEC unaodai kumsimamisha Mbatia kwenye uongozi, ulisimamiwa na Haji Ambari, Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

Ambari anakumbukwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba, kwa kusaliti Zanzibar baada ya kupigia kura Katiba Inayopendekezwa na hivyo, kupatikana theluthi mbili ya kura zilizokuwa zinahitajika

Mbatia Afungiwa Mlango Nyumbani Kwake

 


Mwenyekiti wa chama cha NCCR -Mageuzi James Mbatia na makamu Mwenyekiti (Bara), Angelina Mtahiwa wamesimamishwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili.


Uamuzi huo umefikiwa leo Mei 21, 2022 na Halmashauri Kuu ya chama hicho kutokana na viongozi hao kukabiliwa na tuhuma za kuwagombanisha viongozi kuwalazimisha kujiuzulu na tuhuma nyingine.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio la kusimamishwa kwa viongozi hao Joseph Selasini amesema pamoja na hatua hiyo pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.


“Viongozi hawa wamesimamishwa hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma zinazowakabili na hii ni kutokana na tabia ya kukosa uaminifu,” amesema Joseph Selasini.


Naye Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Sisty Nyahoza amesema tayari amepokea barua kutoka NCCR-Mageuzi ikijulisha mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.


“Pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo hivyo tunasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa,” amefafanua Nyahoza.


Mbatia ni miongoni mwa wanasiasa wachache waliodumu kwenye siasa za Upinzani Tanzania akiwa miongoni mwa wenye viti wenza wa umoja ulioitwa UKAWA uliondwa kwa pamoja na vyama vingine vya upinzani kama CUF na CHADEMA.

Ugonjwa wa Monkey Pox Wahatarisha Ulimwengu

 


Shirika la Afya ulimwenguni (WHO), limethibitsha ripoti ya nchi 12 zilizoonesha matukio 80 ya

uwepo wa ugonjwa wa Monkeypox na kwamba bado wanachunguza madai mengine 50 ya

maradhi hayo na kuonya Mataifa Ulimwenguni kuchukua tahadhari.


Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Dkt. Hans Henri Kluge

imetaja nchi hizo kuwa ni Ujerumani, Sweden, Ubelgiji, Ufaransa, Italia, Ureno, Uhispania na

Uingereza.


“Maambukizi ya ugonjwa huo unaoharibu ngozi pia yamethibitishwa katika nchi za Ulaya,

Amerika, Canada na Australia lakini kwa Afrika unapatikana katika sehemu za mbali za Afrika ya

Kati na Magharibi,” ameongeza Kluge.


Ugonjwa huo ambao unasababisha na virusi kutoka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu barani Afrika unatajwa kutokea katika jamii zilizopo karibu na misitu ya Afrika ya kati na Magharibi kuliko na hifadhi za Wanyama.


Dkt. Kluge amesema matukio ya wagonjwa wa Monkeypox yamegunduliwa katika kliniki

maalumu za magonjwa ya zinaa na kwamba maambukizi hayahusishi muingiliano wa safari

ingawa mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume ni moja ya sababu.


“Hata hivyo dalili za wagonjwa waliogundulika barani ulaya zinaonesha kufanana na zile

zilizoripotiwa siku za karibuni katika nchi za Australia, Canada na Marekani ila hakuna uhusiano wa kimaambukizi kulingana na muingiliano wa wasafiri,” amefafanua Kluge.Mtoto mwenye Monkeypox

Aidha Dkt. Kluge amebainisha kuwa WHO inaendelea kufanya uchunguzi kwa nchi ambazo

ugonjwa huo umeibuka ili kupata taarifa zitakazosaidia ugunduzi wa matukio mengine ingawa mpaka sasa haijulikani kiwango cha maambukizi kilichopo kwenye jamii.


“Kwa sasa dalili ni ndogo na wengi wa walio ambukizwa watapona ndani ya wiki chache bila

matibabu ila ugonjwa huu unaweza kuwa mkali zaidi hasa kwa watoto wadogo, wanawake

wajawazito na watu ambao hawana kinga mwilini.” ameelekeza DKt. Kluge.


Ugonjwa wa Monkeypox huambukizwa kwa kugusana na mtu mwenye vidonda kwenye ngozi,

kuvuta hewa yenye matone ya mtu aliye na ugonjwa huo au maji maji ya mwilini, kujamiiana, au kuchangia vitu na mtu aliyeambukizwa.


WHO inaelekeza kuwa dalili za ugonjwa huo zinaweza kuwa ndogo lakini vipele vinavyotokea

kwenye ngozi huwasha na kuleta maumivu na imetoa wito kwa yeyote aliye na dalili za vipele

visivyo vya kawaida kuwahi hospitali ili kupata ushauri wa watoa huduma za afya.


Bado hakuna tiba maaalum ya Monkeypox lakini chanjo ya ugonjwa wa ndui inatajwa kutoa kinga kwa asilimia 85 kwa kuwa virusi hivi viwili ni familia moja na uwezekano wa kuambukizwa ni mdogo.

FAHYMA: Mimi sijawahi kuwa mbali na RAY VANNY, natarajia NDOA, mahusiano yangu yapo serious sana

 


FAHYMA: Mimi sijawahi kuwa mbali na RAY VANNY, natarajia NDOA, mahusiano yangu yapo serious sana

VIDEO:

Q Chief "Nimeoteshwa Kuwa Mimi Natakiwa Kuwa Mganga"


Ikiwa ni takribani miaka miwili bila kuachia kazi mpya, Q Chief afunguka kurudi kivingine mwezi huu kwa kuachia wimbo mpya ambao una video yake tayari.

Akizungumza kwenye Chill na Sky hapa SnS, Q Chief ameeleza hayo sambamba na kuweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa alioteshwa na kupewa mamlaka ya kutibu watu, karama ambayo anasema alikuwa ameandaliwa kuwa nayo tangu zamani na kwasasa yeye ni Sharif.

Akimjibu Sky kuhusiana na masuala ya kuwa Sharif, Q Chief amesema, "Mimi kitaaluma sio mwanamuziki kwa sababu muziki tu naupenda na kiuhalisia kabisa mimi kazi yangu inahitaji utulivu, kazi yangu mimi haionekani lakini mimi naiona" ameeleza Q Chief na kuongeza, "Hicho ndicho kilichokuwa kina nisumbua muda mrefu sana" - Q Chief akiiambia SnS.

Sambamba na hilo Q Chief ameeleza chanzo cha vita na ndugu zake upande wa baba, vita ambayo aliwahi kuisimulia A-Z katika ukurasa wake wa Instagram.

"Mimi nilikuwa napigana vita ya ndani, vita ambayo ni ngumu sana kwa mwanadamu kuishinda na wengi wameishindwa kwa sababu hujui unapigana na nani. Kuna watu walifunga nafsi yangu, tena kuifunga moja kwa moja, na adui mkubwa wa maisha ni ndugu".

"Nilikuja kugundua tunachopigania na ndugu upande wa Baba ni nguvu na mamlaka na kubwa cha ziada ni karama niliyonayo, ndugu wanahoji kwanini nipewe Karama".

"Nimeamua kuzungumza kwakuwa wanaoumia ni watoto wangu sio mashabiki kwa sababu hawajui nini kinachoendelea juu yangu. Kwa sasa kazi nazifanya kwa mikono yangu yaani najua mimi nifanye sayansi gani kwako ili mambo yako yaende" 

Waziri agoma msamaha kodi kwa gari la kifahari 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Fedha na Mipango, Saada Mkuya Salum,  amesema wizara imekataa kutoa msamaha wa kodi ya Sh. milioni 308.5 kwa gari la kifahari aina ya Benzi.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Fedha na Mipango, Saada Mkuya Salum.
Gari hilo ni la Kampuni ya Turkys Mifuko inayomilikiwa na mfanyabiashara Toufky Salum Turky na kwamba maombi ya msamaha huo yalikuwa kinyume cha Sheria ya Uwekezaji.

Akizungumza na waandishi wa babari ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar, Waziri Saada  alisema msamaha wa kodi kwa wawekezaji unapaswa kutolewa wakati wa ujenzi wa mradi na siyo baada ya mradi kukamilika na kuanza kuzalisha.

“Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, maombi yake ya msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Mifuko Turky yalikataliwa na waziri kwa sababu yameletwa kinyume na sharia, mradi ukiwa tayari umeanza uzalishaji kinyume na sheria.,”alisema Waziri Saada.

Alisema kwa mujibu wa sharia, mwekezaji anaweza kunufaika na msamaha wa kodi wakati wa ujenzi wa mradi, lakini baada ya mradi kukamilika na kuanza uzalishaji, fursa ya msamaha wa kodi inakuwa imemalizika.


 
Alisema kwa msingi huo, ndiyo maana Wizara iliamua kuyatupa maombi ya kampuni hiyo ya kutaka msamaha wa kodi.

“Wizara kazi yetu kubwa kusimamia sheria, taratibu na mifumo hatuwezi kufanya mambo kinyume cha sheria hasa katika suala la kusimamia mapato ya serikali,“ alisisitiza.

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar, Juma Hasssan Hassan, alisema baada ya maombi yao wanatakiwa kurudi TRA kulipa kiwango hicho cha kodi.

Alisema TRA inaendelea kuwafuatilia kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kusimamia sheria ili kuhakikisha fedha hizo zinalipwa baada wa waziri kukataa kutoa msamaha wa kodi wa gari hilo la kifahari.

Kaimu Meneja Uhusiano na Elimu kwa Walipakodi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Makame Khamis Mohamed, alisema gari hilo limesajiliwa na kupewa namba Z-1 kutokana na wahusika kulipa Sh. milioni 15 baada ya kuingizwa Januari, mwaka huu.

Alisema kama gari linatembea mitaani, watakuwa wanavunja sheria kwa sababu hairuhusiwi kutembea kabla ya kukamilisha malipo ya kodi.

Kumekucha..Nabi Atoa Kigezo Kizito cha Usajili Mpya YangaYANGA inalikaribia taji la 28 la Ligi Kuu Bara ikibakiza hatua chache tu na kocha wake, Nasreddine Nabi ametoa masharti mapya ya usajili wake.

Akizungumza na Mwanaspoti Nabi alisema timu yake itahitaji watu wachache wapya kuongeza nguvu haswa kimataifa lakini usajili huo hautampa nafasi staa yeyote ambaye alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila kucheza. Awe wa kigeni au mzawa.

Nabi alisema hawatarudia makosa ya kuchukua mchezaji ambaye hata kama ni bora lakini hakuwa anacheza soka la ushindani kwani muda wa kujiandaa na msimu ujao kwa ndani na kimataifa ni mfupi.

“Ukiangalia ligi hapa itaisha mwezi Juni, tutahitaji muda pia wachezaji kupumzika lakini mapumziko hayo hayatakuwa marefu kutokana na kalenda ya msimu ujao hasa mashindano ya Afrika iko karibu sana,” alisema Nabi ambaye timu yake itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza kati ya Septemba na Oktoba.


“Hali hii sio afya kumchukua mchezaji ambaye alikuwa hachezi soka la ushindani huko anakotoka, tunahitaji kuingiza mtu bora ambaye alikuwa anapata nafasi ya kucheza ili aje kuendelea hapa.

“Kuna uamuzi tuliufanya hapo nyuma umetupa kitu cha kujifunza, mashabiki wetu hawatatuelewa kama tukiendelea kufanya makosa ya namna hiyo, hii ni timu inayoongozwa na viongozi,wanachama na mashabiki wenye kiu kubwa ya mafanikio,” alisema Nabi.

Yanga ilimsajili winga Chico Ushindi kutoka TP Mazembe ambaye licha ya kuwa na kipaji kikubwa lakini kukosa kwake kucheza ndani ya timu hiyo ya DR Congo alishindwa kufanya kazi bora ndani ya Yanga.


Masharti hayo ya Nabi yanamuweka beki wa kushoto wa Uganda, Mustapha Kiiza katika nafasi ngumu ya kusajiliwa na timu hiyo licha ya kuwa chaguo lao kwani amekuwa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya miezi sita.

Mwanaspoti linafahamu kwamba tangu Kiiza asajiliwe na CF Montreal ya Ligi Kuu ya Marekani hakuwa anacheza kwa muda mrefu hatua ambayo kulingana na masharti hayo ya Nabi yanamuondoa beki huyo kulamba dili hilo.

Mapema Kiiza kabla ya kutua CF Montreal akitokea KCCA, Yanga kupitia injinia Hersi Said iliwahi kumuhitaji lakini beki huyo akawapiga kona kisha kuelekea Marekani.

Yanga inasaka beki wa kushoto wa maana ambaye ataondoa changamoto za nafasi hiyo baada ya kuyumba kwa mabeki wao Yassin Mustapha na David Brayson huku winga wa kushoto Farid Mussa akipewa eneo hilo mara kadhaa.

Rais amuapisha Mwalimu aliyemfundisha form 2 na 3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo amemuapisha Mwalimu aliyewahi kumfundisha masomo ya Kiingereza na Hesababu akiwa kidato cha pili na cha tatu kuwa Kamishna wa Tume wa Utumishi wa Umma.

Akizungumza hii leo Mei 21, 2022, mara baada ya kumuapisha, Rais Samia amesema kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa upande wake kumuapishwaa Mwalimu wake huyo.

"Leo nimepata kazi kidogo kumuapisha Mwalimu wangu Bi Khadija, huyu bibi vyovyote alivyo mfupi, mdogo ni mwalimu wangu wa Hesabu na Kiingereza Form Two na Form Three," amesema Rais Samia  

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Wale wa umri kama kina Bi Khadija, wakokoteni hivyo hivyo twende nao lakini ninajua akili iko vizuri, mimi kanifundisha akiwa kijana mdogo na nilikuwa nathubutu kusimama na kumuiga darasana nikijua anaingia basi nakwenda kwenye blackboard na-act exactly alivyokuwa akifanya napengine labda ndiyo maana nimekuwa hivi,".


Breaking News: NCCR-Mageuzi yamsimamisha MbatiaDar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali.

Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR  na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.

 
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.

Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa.

"Tuna orodha yetu tutaenda kuangalia kama mlivyoona wajumbe wapo na akidi imetimia hivyo tunangoja barua rasmi kisha tutaenda kupitia na katiba yao," amesema Nyahoza

CURVES EXTREME ni bidhaa mpya ya kuongeza hips na makalio.


CURVES EXTREME ni bidhaa mpya ya kuongeza hips na makalio. Pia inakaza maziwa yaliyolegea. Dawa hii imesaidia maelfu ya watu duniani, imetengenezwa kwa mimea na matunda tu na haina madhara yoyote. Dozi yake inapatikana kwa ofa ya @270,000/=

N.B hakikisha kuna mhuri halisi wa NATURAL BEAUTY CO ili kuepuka bidhaa feki mitandaoni 

PIA TUNA 👇🏼👇🏼

1. Kuongeza shepu (hips,makalio na mapaja)
Kwa:- 
(a) BOTCHO MULT PLUS (kunywa/kupaka) @270,000/=
(b) vidonge (U/MACCA ORIGINAL) @300,000/=
2. Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) @170,000=
3. Kuwa mweupe bila sugu kwa:-
(a)mafuta @170,000/=
(b) vidonge @220,000/=
4. Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @170,000/=
5. Kuongeza urefu na upana wa uume pamoja na nguvu kwa:-
(a)Gely ya kupaka @200,000/=
(b) vidonge maalumu kwa ajili ya nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na waliojichua @220,000/=
(c)MAX MAN/GOOD MAN na VIMAX ya kuongeza uume na nguvu pamoja na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @270,000/=
6. Kubana uke na kuondoa uchafu ukeni @130,000/=
7. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni @230,000/= 
8. Kupunguza au kuongeza maziwa na kuyasimamisha @180,000/=
9. Kupunguza unene,uzito na manyama uzembe @270,000/=
10. Kuongeza hamu ya kula,unene wastani na uzito @170,000/= 

       Wasiliana nasi popote ulipo duniani kwa call/whatsapp no (+255)

     0759029968 
              na
     0659618585 
UTAPATA HUDUMA 
 
Follow us 👇👇
Google: NATURAL BEAUTY 
YOU TUBE: NATURAL BEAUTY
Instagram: @natural_beauty_prod
Utaona bidhaa zetu na shuhuda za walioitumia 

 FREE DELIVERY IN
*D'salaam
*Arusha 
*Morogoro
*Mwanza
*Moshi
*Katavi

#HipsNaMakalio
#BidhaaTz
#YodiPillsTz 
#BotchoOg
#CosmeticsTz
#WeupeBilaDoa
#FashionsTz
 
LET'S SHINE TOGETHER

      WELCOME ALL

Mfahamu Gangisa Luteni Kanali Mstaafu wa Songea aliyefanyakazi na Idd Amin wa Uganda miaka mitatu


Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa mwenye umri wa miaka 96 ambaye anaishi Chandarua Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma akiwa na rafiki yake hayati  Dikteta Idd Amini wa Uganda

Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa miaka 96 akiwa katika mahojiano maalum nyumbani kwake Chandarua Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

TANZANIA haitamsahau Dikteta Idd Amini Dada aliyeitawala Uganda kwa mabavu kisha kuvamia Tanzania mwaka 1978 ambapo Tanzania iliingia vitani na kufanikiwa kumng’oa mvamizi huyo mwaka 1979.

Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 96 anaishi Chandarua Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma anasema Idd Amin anamfahamu vizuri kwa sababu walisoma na kufanyakazi pamoja kwa miaka mitatu Nakuru nchini Kenya.

Gangisa alizawaliwa mwaka 1927 katika eneo la Ruhuwiko mjini Songea ambapo alijiunga na jeshi la wakoloni mwaka 1947 ambapo mwaka 1953 alikwenda chuo cha Jeshi Nakuru Nchini Kenya ili kupata mafunzo Zaidi ya kijeshi ambako alikutana na Dikteta Idi Amini.


 
“Nimesoma na Idd Amini miaka mitatu kuanzia 1953 hadi 1955 alikuwa rafiki yangu sana,tulikuwa tunalala chumba kimoja bwenini, baada ya kumaliza kozi mimi na Amini tulipata alama za juu hivyo chuo kilitupa makataba wa kuwa walimu tulifanya kazi sote tukiwa na cheo cha Sajenti kwa miaka mitatu’’,anasema Luteni Kanali Mstaafu Gangisa.

Hata hivyo Gangisa anasema licha ya Amini katika kipindi hicho kuonekana kuwa ni kijana mtulivu na ambaye hakuwa mgomvi sana isipokuwa alikuwa mpiganaji wa ngumi na kwamba Amin alimwomba Gangisa amfundishe ngumi,lakini alikataa.

Gangisa anasema kwa muda alioishi na Idd Amin aligundua dosari kubwa aliyokuwa nayo tangu kipindi hicho Dikteta Idd Amin alipenda sana vyeo hivyo hata aliposikia amepindua nchi hakushangaa kwa sababu alimfahamu.

Luteni Kanali Mstaafu Gangisa anasema baada ya kumaliza mkataba wa kufundisha Nakuru alirudi Nyeri nchini Kenya kambi yake ya Jeshi kuendelea na Vita ya Maumau kisha alikwenda kwenye vita nchini Mauritius na Idd Amin alirudi kwao Uganda ambapo mara ya mwisho kuonana na Idd Amin anasema ilikuwa mwaka 1960 nchini Kenya.

Anasema mwaka 1964 alishiriki katika kuunda JWTZ Jeshi jipya lenye heshima nchini Tanzania na kwamba yeye ni miongoni mwa maafisa waliunda JWTZ ambapo yeye ni Ofisa wa 50 wakati huo akiwa na cheo cha Luteni Kanali.

Kwa mujibu wa Luteni Kanali Mstaafu huyo,Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere wakati anaanza harakati za uhuru na kuunda chama cha TANU yeye alikuwa na Idd Amini Nakuru Kenya.

“Idd Amini ndiye aliyenipa taarifa kwamba wewe Mswahili nyumbani kwako kuna bwana ameanzisha Chama cha kupigania uhuru,alinitisha kwamba Maumau itaamia kwenu,nikamwambia Mungu yupo,alikuwa anaongea Kiswahili kizuri,alikuwa rafiki yangu mkubwa sana’’,alisisitiza Gangisa.


 
Gangisa aliacha kazi ya JWTZ mwaka 1978,lakini baada ya kusikia Idd Amini amepindua nchi ya Uganda na kuvamia sehemu ya Kaskazini ya Tanzania aliamua kurudi jeshini kupambana na rafiki yake Idd Amin.

“Nilisema kama amevamia nchi yetu narudi jeshini,tulipambana naye,nilifika hadi kijijini kwake,Kampala pale alinusurika kuuawa, akatorokea njia ya Kenya,tuliwaomba Kenya wafunge mpaka walikataa hivyo Idd Amin akanusurika akatoroka ukiwa ndiyo mwisho wa Vita ya Uganda’’alisema.

Luteni Kanali Mstaafu Gangisa pia anasema alishirikiana na Samora Machel wa Msumbiji wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Msumbiji ambapo mara kadhaa amelala kwenye mashimo na Samora Machel.

Anasema Samora Machel mara baada ya Uhuru alifika Songea mwaka 1975 wakati anazungumza na wananchi alimshukuru Luteni Kanali Gangisa akisema alishiriki naye kwa kutoa silaha na walilala wote kwenye mashimo na kula mihogo ya watu wakati wa mapambano ya wareno.

Gangisa anatoa rai kwa serikali kuwakumbuka wastaafu waliolitumikia Taifa kwa uzalendo mkubwa ili kumalizia kwa furaha maisha yaliobaki hapa duniani.

Imeandaliwa na Albano Midelo


Namna nilivyoweza kuacha kuvuta Sigara baada ya miaka 23

 


Kwa miaka mingi nilikuwa napambana kuhakikisha kuwa naacha kuvuta Sigara lakini hilo lilinishinda kabisa, kuna wakati niliweza kukaa hata wiki moja bila kuvuta lakini nikipita mahali nikasikia mtu anavuta ghafla kiu inakuja. 

Tayari mwili wangu ulikuwa umeanza kupata madhara kutokana na uvutaji Sigari, kila mara nilikuwa nakohoa hasa nyakati  za usiku, jambo hilo lilikuwa linamkwaza sana mke wangu kiasi kwamba aliamua kuhama chumba tulichokuwa tunaishi pamoja.

Nilianza kutumia dawa za mitishamba na kufuata aina fulani ya kanuni za kisaikolojia ili kuweza kuondoka katika kifungo hicho lakini sikweza kufanikiwa. 

Nakumbuka wakati naaza kuvuta Sigara mama yangu aliniambia nitakuja kujutia sana maishani mwangu, aliniambia ukiona hadi kitu kimeandika; (Onyo: Uvutaji wa Sigara ni hatari kwa afya yako) basi jua ni hatari kweli kweli. 

Kutokana na maisha ya ujana kwa wakati ule sikuweza kuelewa hilo, lakini athari nilizokuja kuzipata kama kukohoa sana na kushindwa kumpatia haki yake ndoa mke wangu vilivyo, ndipo nikayakumbuka maneno ya mama yangu. 

Baada ya kuteseka na kuangaika kwa miaka mingi niliweza kukutana na mtu anayeitwa Dr. Kiwanga ambaye naweza kumuita Shujaa wa maisha yangu. Mtu huyu nilipatiwa namba yake (+254 769404965) na mjomba yangu ambaye alisaidiwa na Dr. Kiwanga kupata kazi, aliniambia anaweza kunisaidia nami kuacha kuvuta sigara kwani ameweza kuwasaidi hadi wenye urahibu wa dawa za kulevya. 

Nakumbuka baada ya kutumia dawa za Dr. Kiwanga niliweza kuacha mara moja uvutaji wa sigara na sasa ni miaka miwili sijavuta kabisa na nikisikia harufu yake tu najisikia hata kutapika. 

Kwa kweli kwa sasa hata naweza kusema hali yangu ya kiafya imeweza kuimarika kwa kiasi kikubwa tangu niachane na  uvutaji sigara na hata maendeleo nimeanza kuyaona kwenye maisha yangu. Mke wangu wamekuwa mwenye furaha ndani ya ndoa maana naweza kumtimzia kile anachostahili kupata kama mke wa ndoa. 

Asante sana kwa Dr. Kiwanga kwa uponyaji huu wa ajabu, kumbuka mtu huyu anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha na mengine mengi. Pia ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara. 

Kwa mawaziliano zaidi mtumie barua pepe; kiwangadoctors@gmail.com,


Tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com 


Au piga simu +254 769404965.

Mwisho.

Abiria Wanane Waangamia Katika Ajali Baada ya Dereva wa Basi Kushikwa na UsingiziWatu wanane wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea mapema leo kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu
Ajali hiyo inaripotiwa kutokea baada ya dereva wa basi kushikwa na usingizi na kupoteza udhibiti wa gari kabla ya kugonga nan a lori la kusafirisha changarawe
Miongoni mwa waliofariki ni wanawake wanne na wanaume wanne wanaosemekana kuwa safarini kuelekea katika hafla ya mazishi Kisii
Watu wanane wameangamia katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Nairobi kuelekea Mai Mahiu asubuhi ya Jumamosi, Mei 21.

Abiria Wanane Waangamia Katika Ajali Baada ya Dereva wa Basi Kushikwa na Usingizi
Watu wanane wamepoteza maisha yao katika ajali ya barabarani Jumamosi. Picha: Citizen Digital.
Ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa nane usiku ilihusisha basi la abiria na gari jingine aina ya lori na kuacha watu wengine kadhaa wakiuguza majeraha.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kugonga lori lilokuwa likisafirisha changarawe kuelekea Nairobi.

Mtandao wa Citizen Digital unaripoti kuwa afisa wa polisi ambaye alikuwa eneo la tukio ajali hiyo ikitokea lakini alikataa kutajwa, anadai kuwa dereva wa basi alishikwa na usingizi akiwa kwenye usukani, basi hilo likipoteza mwelekeo na kugongana ana kwa ana na lori lililokuwa likija.


 
Kasri la Baba: Mbili Tatu Kuhusu Jumba la Kifahari la Raila Katika Eneo la Riat Hills
Inaarifiwa miongoni mwa waliofariki ni watu wanane, wanawake wanne na wanaume wanne, wanaosemekana kuwa katika safari ya kuelekea Kisii kwa ajili ya hafla ya maziko.

Ajali hiyo ya saa nane usiku ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu Nairobi, polisi wakilazimika kujitokeza kwa wingi ili kurejesha hali ya kawaida.

Majeruhi walikimbizwa hadi Hospitali ya Naivasha Level 4 kwa matibabu huku miili ya walioaga ikihifadhiwa katika makafani ya hospitali hiyo.

Muda Mwingine Wanaume Kuchapiwa Wake zetu Tunatakaga WenyeweHili suala nimelifikiria kwa kipindi kirefu sana., naona mifano mingi kupitia kwa marafiki zangu na hata ndugu zangu na watu wangu wa karibu. Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana. Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.

Recommended:

READ NECTA RESULTS HERE ( FORM TWO AND FORM FOUR RESULTS


Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Kuna rafiki yangu wa karibu aliwahi kuoa mwanamke wa aina hiyo, ndoa yao ilidumu kwa miaka 5 tu na mimi nilikuwa best man wake, maana mwisho wa siku ikaja kugundulika hata watoto wawili ambao walikuwa wameshazaa hawakuwa wa kwake.

Recommended:


Wanaume tujifunze jamani tunapochagua mwanamke wa kuishi naye kwa maisha yote, tusiziendekeze akili za nyege wakati wa kuchagua wenzi wa maisha.

Nimemuambia Wife Awe Anasuka Style hii ya Nywele ili ku-Save Cost, Kaishia Kunisunya na Kunibinulia Midomo

 


Kwema ndugu zangu watanganyika? Kutokana na mimi kupitia changamoto za kifedha kwa sasa, nilimuomba Wife tupunguze gharama za uendeshaji wa maisha yetu kwa kujibana sana, pendekezo langu la kwanza nilipendekeza Wife anyoe nywele zake alizosuka, akajitetea kwamba nywele zake katumia karibia miaka 10 kuzifikisha hapo zilipofikia hivyo hatoweza kuzinyoa na akaongezea kuwa akinyoa yeye huwa ana kichwa kibaya hivyo hatokua comfortable.

Basi mimi nikajaribu kupitia kwenye baadhi ya pages za wadada wenye saloon huko Instagram nikaja na pendekezo moja kuwa Wife awe anasuka style fulani hivi ya nywele ambayo ni affordable kwani ni elfu 5 tu ila mwenzangu nilipomshirikisha hivyo akaishia kunisunya na kunibinulia midomo kuwa hayuko tayari.

Mpaka sasa kaninunia ila mimi msimamo wangu uko pale pale sitotoa zaidi ya elfu 5 ya kusukia.

Asanteni

By Mdau

Kwanini Baadhi ya Kina Dada Hupenda Wanaume Wahuni na Makatili (Bad Boys) na Kudharau Wapole?

Utakuta kila mara anapigwa anatukanwa na kugundua ana Wasichana wengine lakini yumo tu kazi ni kulalamika kwa mashoga zake, huko watamshauri aachane na huyo jamaa katili na muhuni lakini utakuta anawadharau anaenda tena.

Naamini hili halipo kwa Wakurya tu ni wanawake in general hawapendi watu soft. Kweli hawa viumbe ni wa ajabu sana wakati mwingine si mke wa mtu ni mpenzi tu chuoni ama uraiani hata kwenye mashule wanapigwa tu na kuendelea kuwa na Body Boys

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Wakati mwingine ni kama wanachokoza ili wapigwe maana wakionywa jambo flani wanarudia kisha wanapigwa halafu wanaunda jopo la kuomba msamaha.Je ni Tatizo la Kisaikologia ama ndo Nyota za Punda?

Kutana na Miujiza ya Mtaalam Bahati Kutoka Morogoro


KUTANA NA MIUJIZA YA MTAALAM BAHATI KUTOKA MOROGORO


MTAALAM WA TIBA ASILI TANZANIA NA DUNIANI KOTE

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU MTAALAM BAHATI KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI:


MTAALAM BAHATI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili,

🔥anatumia kitabu cha
quran dawa za asili dawa za kiarabu, na majini,

🔥Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi,

🔥nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k,

🔥anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa pete za bahati, zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote,

🔥pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo.

WASILIANA NAE KWA SIMU NO: +255 719 626 586
WhatsApp no: +255 719 626 586

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa wakati.

FAIZA ALLY anena MAZITO kuhusu SUGU, atoboa siri hii iliyopo moyoni mwa Baba Sasha, Upendo watawala

 


FAIZA ALLY anena MAZITO kuhusu SUGU, atoboa siri hii iliyopo moyoni mwa Baba Sasha, Upendo watawala

VIDEO:

HARMONIZE alilivunja vipande vipande PENZI la BEKA FLAVOUR? Baby Mama wake afunguka A to Z

 


HARMONIZE alilivunja vipande vipande PENZI la BEKA FLAVOUR? Baby Mama wake afunguka A to Z

VIDEO:

Mbunge wa Kenya adaiwa kughushi vyeti vya shule

 


Mbunge wa Kenya ambaye anatuhumiwa kughushi vyeti anadaiwa kuwa hakufanya mitihani yake ya mwisho katika shule ya upili anayodai kuwa alisoma, mwalimu wa zamani shule ameambia mahakama.


Mbunge huyo, Oscar Sudi, alisema kwamba alifanya mitihani hiyo katika Shule ya Sekondari ya Highway mwaka wa 2006. Lakini mkuu wa zamani wa shule hiyo alisema nambari ambayo Bw Sudi alisema ilikuwa yake ni ya mwanafunzi mwingine, na kuongeza kuwa mbunge huyo hakujisajili wala kufanya mtihani shuleni.


Mbunge huyo ameshtakiwa kwa kughushi cheti cha stashahada na cheti cha shule ya upili. Lakini Amekanusha mashtaka na yuko nje kwa dhamana.


Kulingana na gazeti la Standard la Kenya, madai hayo ya kughushi yalianza tangu alipokuwa akitafuta kibali cha uchaguzi mwaka wa 2013 ambapo sheria iliwataka wagombea ubunge kuonyesha uthibitisho wa elimu ya baada ya sekondari.


Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea.

Mwili wa Binadamu Wakutwa Kwenye Njia ya Kurukia Ndege Nigeria

 


Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Nigeria inachunguza baada ya mwili wa binadamu kukutwa kwenye barabara ya kurukia ndege katika uwanja mkuu wa ndege Lagos.

Mtu huyo ambaye hajatambuliwa aligunduliwa wakati wa ukaguzi mapema Alhamisi asubuhi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nigeria imesema katika taarifa yake.

Njia ya kurukia ndege ilifungwa kwa takriban saa mbili na nusu ili kuruhusu maiti kuondolewa, ilisema

Watumishi wa Sekta Binafsi nao Mbioni Kuongezewa Mishahara

 


Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya (TUGHE) taifa bwana Joel Kaminyoge amesema watumishi wa sekta binafsi watarajie kucheka wakati wowote kabla ya tarehe moja mwezi wa saba kutokana na bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi kuelekea mwishoni mwa ukamilishaji wa zoezi la upangaji wa mishahara.


Kaminyoge amebainisha hayo mkoani Njombe alipokuwa kwenye ziara yake ya kawaida ya kuimarisha Chama alipokutana na watumishi ambao ni wanachama wa chama hicho katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe.
“Upandishwaji wa mishahara umefanywa kwenye sekta ya umma,wakati wowote kabla ya tarehe moja july watumishi kutoka sekta binafsi na wenyewe watacheka na hii ni kwasababu kuna bodi mbili za kima cha chini cha mshahara,hii sekta ya umma imeshafanya ndio maana Rais ametangangaza hii sekta binafsi bado wanaendelea kufanya wakati wowote tutasheherekea kwa pamoja”alisema Joel Kaminyoge

Dkt,Apolinary Nombo ni mwenyekiti wa TUGHE tawi la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe ameishukuru serikali kwa kupandasha kima cha china cha mshahara kwa 23.3% kwa kuwa imekwenda kuongeza ari kwa wafanyakazi.


“Tunaishukuru serikali kwa kuongeza hiki kiwango kwa kuwa Mh Rais ametengeneza ari mpya kwa watumishi na kufanya kazi kwa juhudi zaidi”alisema Dkt.Nombo


Baadhi ya wanachama wa Chama hicho ambao ni watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe akiwemo Bariki Mwambije na Neema Hyela wameshukuru Chama hicho kwa kuendelea kupambania haki za wafanyakazi huku wakizidi kuomba vyama vya wafanyakazi kuzidi kupambana na unyanyapaa wa watumishi katika ofisi zao.

Manara Atoa Mpya "Hivi Kwelli Niliwahi Kuwa Simba Sipati Majibu"


Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara @hajismanara amesema hawezi kuwaacha Wapenzi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kwakuwa wamempa heshima kubwa.

Manara amesema kuna wakati huwa anajiuliza kama kweli aliwahi kuwa katika Klabu ya Simba na kushindwa kupata majibu kutokana na upendo anaoupata kutoka kwa Mashabiki wa Yanga.

“Wananchi sitawaacha, hawa wamenipa heshima sana, Klabu hii ni Klabu ya Watu na wakati fulani siku hizi huwa najiuliza hivi Mimi niliwahi kuwa Simba? nilikuwaje! na nikimuona Mtu anashabikia Simba naona huyu aaaaaa!”

Manara yupo Mkoani Njombe kwa mwaliko wa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa @kissagwakisakasongwa ili kutangaza utalii na shuguli mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika Wilaya hiyo.

Baba Levo: Harmonize Hawezi Kumzima Diamond “Ni Mtoto tu Anayejaribu Kuiga”BABA levo au Mtaalam Fundi Manyumba; ni msanii wa Bongo Fleva, komediani na mtangazaji wa Wasafi ambaye amemchamba msanii Harmonize kwa mara nyingine na kusema kwamba mkurugenzi huyo wa Konde Music Worldwide hana uwezo hata chembe wa kumzima Diamond Platnumz kwa lolote iwe kimuziki au hata kufanya kiki.

Kwa mujibu wa Baba Levo, Harmonize bado hajai hata kwenye kiganja cha Diamond au Mondi kwani ni kama mtoto tu anayejaribu kuiga baba’ke wa muziki, lakini ameshindwa na kuamua kutumia njia hasi ya kutembeza chuki na matusi dhidi yake mitandaoni badala ya kujitahidi kumfikia na akishindwa kumfikia basi arudi kujiunga naye na kumshabikia.


Mkurugenzi wa Konde Music Worldwide, Harmonize.
“Harmonize hana uwezo wa kutengeneza kiki ya kumfunika Diamond Platnumz, kwa vyovyote vile hana uwezo wa kuzima EP ya FOA,” anasema Baba Levo.

Chawa huyo wa Diamond au Simba anatilia mkazo kwamba amesema mara nyingi tu kwamba si Harmonize pekee, bali msanii yeyote atakayedanganyika akajaribu kushindana na Diamond, basi atapoteza vingi; yaani itakuwa kama ng’ombe anayejaribu kushindana na ndovu, bila shaka atakwama kwenye gogo la tembo.


 
“Nimeshasema mtu yeyote atakayejaribu kushindana na Diamond ataishia kupoteza vitu vingi,” anasisitiza Baba Levo.

STORI; IJUMAA WIKIENDA, DAR

Exclusive… Mama Dangote Amlipukia Zari, Acharuka Baada ya Kuulizwa Juu ya ujio WakeSanura Kassim almaarufu Bi Sandra au Mama Dangote; ni mama mzazi wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz ambaye amejikuta akicharuka na kulipuka baada ya kuulizwa juu ya ujio wa mzazi mwenza wa mwanawe huyo, Zarinah Hassan au Zari The Boss Lady ambaye ametua Bongo wikiendi iliyopita bila kukanyaga kwa mama huyo.

Zari alitua Bongo akitokea nchini Afrika Afrika Kusini, lakini hakutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, badala yake aliunganisha ndege na kwenda kutua jijini Mwanza kabla ya kesho yake kuonekana akijiachia kwenye kiwanja cha bata cha Beach-Kidimwi jijini Dar.

Akiwa jijini Mwanza, Zari alifanya shughuli zake za kijamii kama kawaida yake akiwa ni balozi wa bidhaa za taulo za kike.

ZARI ASHAMBULIWA

Ujio huo wa Zari ulidaiwa kuibua makasiriko kwa baadhi ya Wabongo ambao walihoji kitendo cha mwanamama huyo kutua Bongo na kushindwa kufika nyumbani kwa kwa Diamond Platnumz, Mbezi-Beach au kwa Mama Dangote kule Madale ilihali aliweza kwenda kujiachia Kidimbwi.


 
Zari amejikuta akishambuliwa kwa kujiita wifi na shemeji wa Watanzania, lakini akashindwa kufika nyumbani kwa Diamond na wakwe zake kuwajulia hali hivyo kuhojiwa huo uwifi na ushemeji wa aina gani?


Sanura Kassim almaarufu Bi Sandra au Mama Dangote.
Hata hivyo, wengine walikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, Zari alikuwa wifi na shemeji kipindi kile akiwa na Diamond na siyo sasa ambapo kila mmoja amechukua hamsini zake na si lazima kila akitua Bongo, basi aende nyumbani kwa jamaa huyo au kwa Mama Dangote.

MAMA DANGOTE ALIPUKA

Baada ya sakata hilo kugeuka mjadala wa kitaifa, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Mama Dangote ambapo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo aliwaka ile mbaya;


“Kwani kila akija lazima niwatangazie? Wao wanataka wafahamu kama nani? Kwani akija huwa ninawapa taarifa kwamba amekuja? Hao wanahoji ni kama nani? Ninyi andikeni mnavyotaka kuandika,” anasema Mama Dangote kwa hasira.

ZARI AJIBU MAPIGO

Kwa upande wake, mwanamama Zari ameibuka kuhusiana na wanahoji juu ya ishu hiyo na kujibu mapigo kwa kuwapa za chembe wale wote wanaomfuatilia yeye na maisha yake.

Zari anasema; “Unajua Watanzania wengine mimi siwaelewagi, nisipoenda Madale (nyumbani kwa Mama Dangote) au Mbezi (nyumbani kwa Diamond) wanasema ooh hawamtaki, hawaotaki kuonana naye.

“Nikienda wanasema Zari anapenda sana kuiganda na kujipendekeza kwenye hiyo familia.


 
“Nikienda wanaongea, nisipoenda wanaongea, sasa mtu afanye nini?

“Mimi hao watu (familia ya Diamond) ninaongea nao, nimefika nikawaambia hivi na hivi nimekuja kikazi, wakasema sawa Mama Tee enjoy.

“Sasa wewe unaumwa eti Zari hajaonana na Mama Dangote, kwa nini? Zari hajaonana na ile familia, kwa nini? Wewe unafaidika nini mimi nikionekana na Mama Dangote au mnataka nipigepige picha nirushe kwenye Instagram?

“Mimi siishi maisha ya Instagram. Inaweza kuonekana ni hivyo, lakini siyo hivyo, so I’m sorry (samahanini) mmekuwa disappointed (nimevunjika moyo), lakini ndiyo hivyo,” anasema Zari naye akiwa amepaniki ile mbaya.


ZARI NA WABONGO

Kwa muda mrefu, Zari amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya Wabongo ambao kwa mujibu wake, wana makasiriko kutokana na kuzaa na Diamond kisha akaachana naye hukuakiwa vizuri kimaisha.

Hata hivyo, pamoja na hayo yote, Zari anasema; “Ni Kweli nimeachana na Diamond, lakini ninaipenda Tanzania…”

Stori; Khadija Bakari, Dar

Halima Kopwe Kutoka Mtwara Ametangazwa Miss Tanzania 2022


Halima Kopwe (23) kutoka Mtwara ametangazwa Miss Tanzania 2022 usiku huu Mlimani City Dar es salaam akichukua taji hilo kutoka kwa Rose Manfere Miss Tanzania 2021, zawadi atazopewa Halima ni gari aina ya Mercedez Benz na Tsh. milioni 10 cash. #MillardAyoUPDATES

Yanga Sc imebakiza Mechi Mbili Kuweza Kutangazwa Bingwa wa Ligi ya NBCKLABU ya Yanga imeondoka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Mbeya Kwanza, gimu ambayo inashika mkia kwenye ligi ya NBC.

Ni Fiston Kalala Mayele, baada ya mechi nne mfululizo kukosa kufunga bao leo ameonesha kuwa anaweza mara baada ya kupachika bao la kwanza kwenye mchenzo huo na kufikia mabao 14 akiwa sambamba na mchezaji wa Geita Gold George Mpole.

Yanga Sc imebakiza mechi mbili kuweza kutangazwa bingwa wa ligi ya NBC ambapo mpaka sasa anaongoza ligi akiwa imejikusanyia pointi 63 nyuma ya Simba Sc mwenye alama 50.

Mabao mengine ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na Said Ntibazokiza, Dikson Ambundo na bao la mwisho likifungwa na Makambo.

5/20/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Mbeya Kwanza Ikifa Bao Nne"
1: 4G! MNARA UMESOMA KILELENI✊ YANGA IMESHINDA, MAYELE AMETETEMA. Ni usiku mwingine unaovutia kwenye kitanda cha kila Mwananchi!

2: NABI ametuma ujumbe wake mgumu kwenye kikosi. LENGO NI TIMU SIO MCHEZAJI BINAFSI. Ni kama ilivyokuwa kwa Conte na SON. Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.

3: Tactically, Sure Boy Ni PLAN B bora kwa Yanga kwenye mfumo wao. Kwa muda mrefu Yanga walikuwa na muundo wa 4-2-3-1 Lakini SURE BOY amempa NABI kiburi cha kwenda na 4-3-3! Kivipi?

4: Ubora wa SURE BOY kwenye kupiga
pasi sahihi/kwa haraka unaifanya Yanga iwe na muunganiko na Balance nzuri kwenye kushambulia.. What A Player! Direct Wingers wa Yanga [Ambundo/Moloko] wanaenjoy zaidi Mfumo huu kutokana na huduma wanayoipata katikati ya Uwanja

5:MBEYA KWANZA wamehukumiwa na QUALITY. Ndani ya Uwanja na kwenye Benchi la Ufundi. Yanga walikuwa mbali mno. Kipindi cha kwanza ni kama walikuwa na aibu na kutoelewa nini kinaendelea uwanjani.. Yanga wakawaadhibu haraka haraka

6: Kipindi cha Pili Mbeya Kwanza waliamua kufunguka. Ni kama walikubali kucheza bila 'Details' nyingi vichwani. Wakaja kwenye TOTAL FOOTBALL. Bahati mbaya YANGA WALISHAMALIZA JAMBO LAO!

7: DIARRA NI JINI.. QUALITY. Bonge la Kipa. Sio kwa ajili ya kucheza tu na miguu.. Mikono yake iko imara pia. Ni mechi mfululizo sasa anafanya SAVES za Thamani kupambania Idadi ya CLEAN SHEETS ZAKE.

8: KUNA SURE BOY.. KUNA AUCHO! Utachagua kwa uelewa wako nani anastahili kuwa Man of The Match.. Miguuni mwao mpira ni mchezo rahisi sana! Ni ndoto ya mshambuliaji kucheza mbele ya kiungo mwenye jicho zuri la kuona nafasi na kupiga pasi sahihi

9: Habib Kiyombo.. Well Done! Lakini yule Hamis Kanduru ni kama alikuja kuweka sokoni kipaji chake.. What A Player! Alikimbia, alikokota, Alipiga kila alipopata nafasi. WENYE MACHO WAMEONA 👏

10: Well Done Ambundo. Napenda kujiamini kwake kwenye maamuzi ndani ya Eneo la mwisho. Kazi nzuri Shomari Kibwana.. Lakini Farid Mussa anastahili heshima yake!

Nb: Walichobakiza ni Ubingwa wa kumshangilia Mpole 😃

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger