BABA YAKE LANGA AONGEA-KILICHOMUUA LANGA HIKI HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Baba mzazi we Langa, Mangisemi Kileo ameeleza chanzo cha kifo cha mwanaye ambaye kimetokea jana katika Hospitali ya Muhimbili.
Langa amefariki dunia jana katika hospitali ya Muhimbili baada ya kulazwa usiku wa kuamkia jana.
Imeelezwa Langa alifikishwa hospitalini hapo akiwa amezidiwa na moja kwa moja akafikishwa katika chumba cha watu mahututi.
Salehjembe ilifika nyumbani kwao marehemu eneo la Mikocheni Regency dakika chache baada ya taarifa za msiba na kuzungumza na baba yake mzazi, Mengiseni Kileo.
Kileo alisema Langa alizidiwa ghafla juzi, wakamkibiza katika Hospitali ya Kairuki.
“Pale walituambia kwamba anasumbuliwa maralia kali pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo.

“Hivyo tukalazimika kumkimbiza Muhimbili ambako alifikishwa katika chumba cha watu matuhuti (ICU), leo ndiyo mauti yamemkuta,” alisema.

Kuhusiana na mazishi, Kileo alisema wanalazimika kumsubiri mkewe, Venus ambaye anatarajia kutua nchini kesho au keshokutwa.

“Mama yake yuko Marekani, hivyo tutamsubiri lakini tumeshazungumza naye.

“Sisi tutakaa leo kujadili suala hilo na wanafamilia na baadaye tutajua kila kitu,” alisema Kileo akionyesha utulivu.


Langa alikuwa akitamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki wa Kweli iliyotengenezwa katika studio za Bongo Record chini ya P Funk.
Msanii huyo alianza kutamba baada ya kushinda usakaji vipaji chini ya Coca Cola na kuunda kundi la Wakilisha akiwa na Shaa au Sarah na Witness wakianza na wimbo wao wa kwanza ‘Hoi’.
na global publisher
 
 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad