DIAMOND PLATNUMZ AWAPONDA BARAZA LA SANAA LA TAIFA -BASATA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diamond Platnumz amelishukia Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kuwa linaurudisha nyuma muziki wa Tanzania kutokana na kutoruhusu kuanzishwa kwa tuzo zingine za muziki nchini tofauti na Kilimanjaro Music Awards
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM leo, Diamond amesema hatua hiyo inamfanya ahisi kuna kitu kimejificha ndani ya baraza hilo.

“Kwanini Tanzania tuna tuzo moja, ni kitu ambacho kinanisikitisha sana kwasababu ukiangalia hata nchi zingine ni ndogo sisi tumewazidi kimuziki lakini zina tuzo zaidi ya moja,” alihoji Diamond.

“Sijui BASATA kuna nini kinaendelea.”

Amesema kungekuwepo na tuzo za aina mbalimbali za muziki nchini, kungekuwa na changamoto chanya kwa waandaji wa tuzo hizo kuliko hivi sasa ambapo KTMA haina mpinzani.

“Kukiwa na tuzo tofauti hawa watajifunza kupitia wale, lakini kitu kikiwa kimoja kila siku vinapelekwa tu.”

Kwa upande mwingine Diamond amesema baada ya nominations za Kili kutoka, hakuweza kuongea chochote kwakuwa aliona aliwekwa kwenye vipengele ambavyo hakustahili.

“Ukitazama kabisa kama sikuwa katika category yeyote naweza vipi kuwa msanii bora wa kiume, kwa kigezo kipi,” alihoji.

“Sasa unaniambia mimi sina sifa ya kuwa mbunge, diwani, waziri, sina sifa hizo halafu ukanishindanisha urais sasa ntashinda vipi kama huko mwanzo tu siwezi.”

“Nikaona you know what bora nipige zangu kimya sikutaka kuongea kwasababu hawachelewi kukutafsiri vingine, ndio maana sikuwepo siku zile, kiukweli kabisa.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unachoma dogo ni kweli, haiwezekani msanii bora Wa kike 2012 Bongo fleva hajawahi toa ngoma yoyote ikabamba mwaka huo halafu anakuwa bora na category yoyote hayupo . Hata upande Wa hip hop mtu kuwa msanii bora Wa hip hop kwa mwimbo mmoja tu kutwaa tuzo 3 ai sahihi. Basata waruhusu ili kuleta ushindani ni uhuni mtupu. Halafu wewe diamond mi nawashauri na wenzako kwanini mnakubali kilimanjaro beer kuwatembeza halafu watu wanaingia kuwaona kwa 2500 mnajishusha hadhi

    ReplyDelete

Top Post Ad