Aibu! Vunja Jungu yamtokea Puani Njemba…Anaswa akila URODA na Mke wa Mpangaji wake GESTI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.

Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake.

OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa msimamizi wa gesti hiyo kufuatia  baba mwenye nyumba huyo kukahidi kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani na mzee huyo.

Walidai kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.

Ilidaiwa kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa  akimtaka mke wake kimapenzi.
Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.

“Nilimwambia mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume huyo.

Baada ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.

Shauri hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji. Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.

CREDIT: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Apigwe risasi za pumbu nae...hahahahaha

    ReplyDelete
  2. hivi ukishamfumania mumeo halafu umpeleke police halafu akitoka unamsamehe na anaendelea kuwa mumeo? au inakuaje

    ReplyDelete

Top Post Ad