11/16/2014

Kwa Matokeo ya Utafiti wa TWAWEZA...Hata Diamond Platinum Aweza Kuwa Rais

Nimekuwa nafuatilia kipindi cha asubuhi hii katika kituo cha TV cha StarTV. Nimewasikiliza wote. Huko Dar es salaam Dr. Kitila Mkumbo kaonesha upeo wake katika hili na Mwanaharakati Lenatus Mkinga ameonesha uwezo wake.

Kilicho nishangaza leo Kitila amepwaya sana kwa kutoa hoja zisizo na mashiko kwa kuegemea kumponda Dr. W. P. Slaa kwa kumwita hana adabu kwa kutokubaliana na matokeo hayo ambayo yamempa ushindi Edward Lowasa.

Kitila ameonesha kutokuegemea upande wowote pale alipotamka wazi kuwa utafiti huu una lengo la kumshafisha mtu fulani na ndiyo maaana watu walifanya sherehe ya kupongezana. Kaenda mbali na kutaja kuwa kundi hilo lililosherehekea ndilo hilo hilo lililompatia Dora 2500 cash ili aandae kipindi kwenye TV kwa lengo la kumsafisha mtu wao. Alizichukua fedha hizo na kuziwasilisha kwa viongozi wa CCM na kusema nimepewa fedha hizi kwa lengo la kumsafisha EL. Ameongeza na kusema kuwa utafiti huu umelenga kwenye muonekano wa mtu na sio utendaji au uadilifu katika taifa. Anasema unawezaje kumpa mtu ushindi MWIZI WA MABILIONI YA WATANZANIA kwa kuandaa kampuni fake ya RICHMOND isiyokuwa na usajili wala leseni!!!!!

Ameongea mengi lakini kubwa kuliko ni pale aliposema kwenye orodha ya washindanishwaji kama angewekwa DIAMOND PLATINUM nae angepata kura za kutosha kama vile walivyopata wengine ambao hata kutangaza nia hawajatangaza mf. Tundu Lissu na Magufuri achilia mbali Zitto na wengineo waliotangaza.

My Take:

Dr. Kitila Mkumbo usimlaumu Dr. Slaa kwa wewe kujiita msomi na kumdharau Dr. Slaa kwa kumuita hana adabu. TWAWEZA ninaijua haswa chimbuko lake na sio kama unavyotaka watu tuamini kuwa ni asasi ya kikanda. Pia unanipa mashaka na U-Dr wako kwani kwa sasa unavyoonekana huna tofauti na Prof. wa Kichina....... Jirekebisha Brother unapotea....

By Alfred Daud Pigangoma
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger