Usione Mwanaume Katulia Kwenye Ndoa Ukajua Kaendewa kwa Mganga, Uganga Tunao Wenyewe

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Jana tulikua na kamjadala karefu kidogo kuhusu hawa wandugu kitu gani wanataka ili watulie ndoani. Nami nimeyachuja, nikaongeza na tu chumvi kidogo ili kunogesha. haya si maneno yangu. Ni yakwao wenyewe. Mwenye macho na asome na mwenye kusikia asikilize sauti yake mwenyewe ikisoma....... Usione mwanaume katulia na mkewe ukaanza kuuliza mke kamwendea kwa mganga yupi,uganga tunao wenyewe wanawake shutu kuwajibika;

1. Kumjali mumeo kadri uwezavyo. Usipo mjali wengine wataja saidia kumjali. Mfano …..kuna watu hapa hata hawajui leo mume wake kava nini!! Wengine hata soksi za waume zao haawajui ziko ngapi. Mume anaenda kazini hata hukumbuki kava shati rangi gani. Akipita na kimada mbele yako unaanza kujiuliza, sijui ndo Yule……. Mbona shati ka lake??? Hivi leo alivaa shati ile eh……! Jipange mwanamke

2. Jifunze kuhusu mapenzi na mbinu mpya…. Hii nadhani wanasema ubunifi uwe mara dufu hasa chumbani. Sio mbaya hata mkizungumza na wanawake wenzenu mkapata maujuzi mapya. Style zile apendazo mumeo ndo mwake. Basi hata japo uliza mume wangu vipi hii… nah ii je!! Na Msijisahau, yale masham sham ya uchumba yaendelee mpaka kwenye ndoa.

3. Tuwaelewe waume zetu kutokana na hali zao. Mfano kachoka, anamatatizo. Usiwe wakati wa sisi kuanza lawama. Mume kapata msiba, wewe ndo unapeleka shida zako. Atakuona hovyooo kabisa.

4. Usafi wa nyumba, mwili mzima bila kusahau kinywani. Na uvae vizuri uvutie. Hapa hasa ni usafi na kujipenda. Usione uvivu kujipamba ukiwa kwako na mumeo. Shurti bi mdachi unukie vizuri. Chmba chako sio kinanuka mikojo ya mtoto. Na wanao pia wawe wasafi jamani.Mume anazidi kupata hamasa ya kuwa karibu na familia. Mjitunze vizuri kipindi cha uzazi…. Sio mnanuka maziwaaaa. Yani mazingira yooote yawe ya kushawishi. Nyumbanyingine ukikanyaga tu sakafu, mchaka kama upon je.

5. Jikoni pia uwe mbunifu. Na upate nafasi ya kumpikia mumeo chakula wewe mwenyewe sio kila siku dada wa kazi ndo mpishi. Mume asipate hamu ya kula baa. Kama ni mpenzi wa pombe basi aishie kunywa tu, msosi ataupata kwa mkewe.

6. Kelele majumbani. Hapa wanawake tuache midomo. Kitu kidogo maneno kibao. Kila saa wewe tu ndo unaekerwa. Huishi lawama. Mara nyingine tuchague kukaa kimya, au hata kama tunasema basi kwa sauti ya chini. Si vizuri kumpandishia mumeo sauti hata kama kakosea sema nae tara tara. Na tone zetu ziwe zile za mahaba. Sio umekaza sauti ka unaamrisha gwaride mweh!!!

7. Mnapokosa mkubali makosa na muombe msamaha. Wanaume wanapendaga kuonekana wao ndo kichwa na wanaheshika. Sio unarekebishwa tabia na mumeo, unaishia kununa siku tatu ndani hapaeleweki. Umenunaaaaa hatari.

8. Msijibweteke. Maisha ya sasa ni kusaidiana. So jishughulishe mtoto wa kike. Ukiwa na kakitega uchumi kako si mbaya. Hata mume anakuheshim.

9. Mnapokuwa na watoto mjitahidi kugawa muda kwa ajili ya mtoto na kwa ajili ya mumeo pia. Na msiwe wavivu kutoa unyumba kisa una watoto

kama kunanililo sahau ongezea.......

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
 1. kwa somo lako duuuuuu halina kuongeza

  ReplyDelete
 2. WAAMBIE HAO WANAJIDAI LIBWATA LIMBWATA!!! HAKUNA KITU KAMA HICHO NI WEWE MWENYEWE TU NDO LIMBWATA

  ReplyDelete
 3. Je , na wala waume amabyo unafanya hayo yote lakini ukitoka tu nje ya nchi basi kapata nafasi na hata kuzaa na akazaa,, utafanya je??

  ReplyDelete
 4. Maneno mazuri ila kuna wanaume wengine wanagubu na mambo yao, unaweza ukamfanyua yooooote hayo ila bado ikawa tatizo nao wajiengalie isewe kila kitu mwanamke ndio sababu

  ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad