Harmonize Atoboa Siri 'Ni Kweli Zari Hassan Ndio Aliniunganisha na Huddah Baada ya Kumtamani Kwa Muda Mrefu'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siri nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.

Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, wikiendi iliyopita, Harmonize alisema kuwa kwenye maisha yake hakuwahi kuwa na ndoto ya kukutana laivu na Huddah lakini bahati hiyo aliipata akiwa nchini Afrika Kusini baada ya kukutanishwa naye na Zari.

“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa na Global TV Online.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bwajabwaja nyingii, utafikiri kaenda mwezini.

    ReplyDelete
  2. Tunataka maendeleo sio abari za mashangingi wachunaji

    ReplyDelete
  3. Harmonize kuna magonjwa huyo mwanamke keshapitia wengi sana tena narudia wengi sana. Na wala sio sifa kujisifia umetembea na mtu ambaye anajiuza kila mtu anajua huyo mwanamke anajiuza mpaka ulaya

    ReplyDelete
  4. Kwani ukiwa katika hiyo label ni lazima kutafuta umaarufu kupitia wanawake? Msiigane katika ujinga

    ReplyDelete

Top Post Ad