Ticker

6/recent/ticker-posts

Imeniuma Sana, Mke Wangu Anatembea na Baba yake Mdogo

Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni
By bullar/JF

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

2 Comments

  1. Kisasi cha nn kaka we fuata ustaarabu wako huyo hakuafai huna haja ya kuhangaika na visasi kaa tulia ulee mwanao wakati unatuliza akili kutafuta mwanamke mwingine aliyetulia mkiendana tangaza ndoa...ye muache ulimwengu utamfunza wala huna haja ya kushindana nae...sahiv jiweke bize na kazi za kukuletea maendeleo na kipato yo still young and energetic dont waste yo time to a crap who doesn't deserve you...all the best

    ReplyDelete
  2. tafuta mke mwingine huyo hakufai anaweza kutembea hata na baba yako mzazi km kaweza kutembea na baba yake mdogo. mungu atakupa wa kwako na utasahau kila kitu. lakini atakukumbuka baadae na huyo baba wala hawatakaa milele watabwagana tu hizo ni starehe tu zinamsumbua. fanya yako kaka msahau. mapito tu hayo. mke wako yupo mungu aliytekupangia.

    its me rehema

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)