40 Ya Mdogo Wa Tiffah Usipime, Mastaa Wakubwa Afrika Watajwa Kuhudhuria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

STORI: GABRIEL NG’OSHA, GAZETI LA UWAZI, TOLEO 1021, JANUARI 3-9, 2017

DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa ndani ya familia ya Diamond zilieleza kuwa, Nillan ambaye ni mdogo wa mtoto wa kwanza wa staa huyo, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ anatarajiwa kufanyiwa shughuli hiyo kubwa ya kumtoa ambayo itafanyika nyumbani kwa jamaa huyo huko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Taarifa nyeti zilieleza kuwa, tayari baadhi ya watu wao wa karibu Bongo wamefikishiwa kadi ambapo watakwenda Sauz na kurudi kwa usafiri maalum wa ndege ambapo kila kitu watakuwa wameshalipiwa.

“Tayari Diamond ametoa kadi maalum kwa watu wake wa karibu. Waliopewa kadi wanatakiwa kuthibitisha kama watahudhuria ili kuweka mambo sawa na kujua idadi kamili ya watakaokwenda kwa ajili ya kuwagharamia.

 Mtoto wa kwanza wa Diamond, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’  akiwa kalala na   Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ .

“Unaambiwa siku hiyo (Januari 16), watu watakula bata la kufa mtu maana shughuli ya Chibu Junior itaifunika ile ya Tiffah.

“Mbali na mastaa na watu wa kila aina kualikwa kutoka Bongo lakini pia 40 ya Chibu Junior itahudhuriwa na mastaa wakubwa Afrika ambao wengi ni rafiki zake Diamond hasa wa kutoka Nigeria,” kilifunguka chanzo chetu kikiomba chondechonde kisitajwe popote.


Mbali na chanzo hicho, mtu mwingine ndani ya familia hiyo alipoulizwa juu ya taarifa za mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuhamia Sauz kwa ajili ya shughuli hiyo alisema kuwa, si kwamba tu amehamia lakini kwa sasa mzaa chema huyo ameshakuwa mwenyeji wa mitaa ya Johannesburg kufuatia kuwa huko tangu alipojifungua mkwewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Desemba 16, mwaka jana.

Hata hivyo, alipotafutwa Diamond hakuwa hewani ambapo mmoja wa wanafamilia alisema kuwa yupo nyumbani kwake Sauz kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2017.

“Jamaa hayupo Bongo labda umcheki kwa WhatsApp, yupo Sauz home kwake si unajua mambo ya bata za sikukuu ya mwaka mpya? Kwani kuna ishu gani?,” alihoji mwanafamilia huyo kwa sharti la kutotajwa kwani siyo msemaji wa familia ya Diamond.

Alipoulizwa juu ya 40 ya mdogo wa Tiffah na kwamba kuna mwaliko maalum na itakuwa bab’kubwa, jamaa huyo alifunguka:

“Ebana hiyo shughuli achana nayo kabisa lakini unachotakiwa kujua ni kwamba itampaisha Chibu Junior Afrika nzima.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tushazoe uongo wao. hautushtui. ila wasisahu kulipa makapeti ya shughuli.

    ReplyDelete
  2. Na Irene akizaa atafanyiwa shughuli kubwa kama ya mke mwenza? au Esma ataenda peke yake.

    ReplyDelete
  3. pole Ajuza kuna 3. yuko njiani.

    ReplyDelete
  4. mmekosa vya kuandika?what wastage of time!!!

    ReplyDelete
  5. Dogo kazaliwa December 6 siyo 16, uandishi wa chooni bana!

    ReplyDelete

Top Post Ad