Siku Chache Baada ya Kifo cha Ivan..Zari Kulipwa Mabilioni ya Pesa na Kampuni za Bima..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakati wanafamilia wakiwa bado katika majonzi kufuatia kifo cha mpendwa wao, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyezikwa wiki iliyopita huko Nakalilo nchini Uganda, imebainika kuwa aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ atalipwa mabilioni ya fedha kutokana na bima na mikataba mingine mingi aliyoingia jamaa huyo enzi za uhai wake.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini Uganda, Zari ndiye mtu pekee atakayesimamia mali zote zilizoachwa na Ivan, hasa kutokana na ukweli kuwa ana watoto wake watatu wa kiume na ndiye aliyeanza kutafuta mali wakiwa wote mwanzoni mwa miaka ya 2,000.

KULIPWA NA KAMPUNI YA BIMA

Kwa mujibu wa habari hizo, Zari ambaye alishiriki mwanzo mwisho msiba wa mumewe huyo wa zamani, atapata fedha ambazo Ivan alilipia bima yake ya maisha ambazo hata hivyo, mama huyo wa watoto watano hakuweza kutaja jina la kampuni hiyo ya bima wala kiasi cha fedha atakazolipwa zaidi ya kusema tu ni mabilioni.

“Ivan ameacha mali za kutosha na of course pia alikuwa na bima ya maisha ambayo alikuwa akilipa fedha kila mwezi, kwa hiyo kwa kuwa amefariki dunia, basi nina uhakika wa kupewa fedha hizo ambazo ni nyingi, sina uhakika ni ngapi kwa sababu bado sijapiga hesabu, lakini ni a lot of money,” alikaririwa mwanamama huyo.

BIMA YA MAISHA NI NINI

Bima ni mfumo wa kulipa kiasi cha fedha katika kampuni ya bima ili kujiinua au kujilinda na madhara ya tukio lolote baya litakalotokea katika kitu ulichokatia bima. Kampuni ya bima inachukua jukumu la kurudisha hali iliyochafuka kuwa safi katika mazingira yoyote ya mtu aliyekata bima kwao.

Baadhi ya kampuni zinazotoa bima hiyo ya maisha, mteja huweza kuwa na nafasi ya kukopa baada ya mwaka wa tatu wa ulipiaji wa bima hiyo na bima hukomaa baada ya muda uliolengwa kufikia (mfano endapo mteja alikata bima ya maisha ya miaka 15, tuseme shilingi 150,000 kwa kila mwezi) baada ya muda huo kufika atalipwa kiasi chake chote cha fedha alizoweka, pamoja na faida isiyopungua asilimia tano kutegemea na kampuni.

Endapo mteja atafariki dunia kabla ya muda huo kufika na bila kupatwa na madhara mengine yaliyo katika ulipiaji wa bima, mrithi wake ndiye atapaswa kupewa fedha hizo pamoja na faida.

AMEJIPANGAJE NA MAISHA YAKE?

Zari alisema kuwa, anaamini atapambana kiasi cha kutosha kuweza kuwapa watoto wao watatu vitu muhimu katika maisha yao, ikiwemo elimu, afya, chakula na malazi.

“Kuna vitu vya msingi ambavyo watoto ni lazima wavipate na watavipata kwa sababu baba yao ameacha urithi wa kutosha tu. Mimi siyo aina ya mwanamke ambaye baada ya hili jambo kutokea labda nitahitaji magari au nini sijui, nitahakikisha wanapata elimu nzuri kama baba yao alivyopania kuwapa.

“Uzuri ni kwamba baba yao alishawawekea misingi ya maisha yao kwa hiyo halitakuwa jambo geni kwangu wala kwao. Ninamuomba Mungu tu abariki kila jambo liende vizuri na kwa kweli tunaomba sana.

MALI ZINGINE ZITAKAZOBAKI MIKONONI MWA ZARI

Kwa mujibu wa Zari, aliyenukuliwa na mitandao ya nyumbani kwao Uganda, yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa vyuo na shule zote zilizoko Afrika Kusini, ambazo zilikuwa zikimilikiwa na Ivan.

“Kuna manenomaneno mengi yanasemwa na watu, akiwemo baba mdogo wa Ivan, wanasema mimi ninagombea mali, siyo kweli, kwa nini nigombee, wasichojua ni kwamba mimi ndiye nilianza kutafuta mali nikiwa na Ivan hadi tukapata na hawajui kuwa hata baada ya kutengana, bado alikuwa kila siku akitaka nirudi ili nisimamie mali maana aliona zinaanza kupotea.

“Kuna nyumba moja ambayo tulijenga ikiwa na majina yetu mimi na yeye na nyingine ilikuwa na jina lake kila kitu. Hivi vitu vyote vitakuwa chini ya usimamizi wangu kwa ajili ya watoto hawa ambao wanahitaji kupata mambo yote muhimu,” alisema Zari.

ANA MATATIZO NA FAMILIA YA IVAN?

“Sijawahi kuwa na wala hakutakuwa na matatizo kati yangu na familia ya Ivan, kule kuna wajomba, shangazi, dada na kaka za watoto wake, ninahitaji sana kuwa nao karibu na nitahakikisha kila jambo ninawashirikisha.

“Ikitokea nikashindwa kulipa ada ya watoto nitawaambia jamani nisaidieni nimeshindwa. Lakini siyo hivyo tu, hawa watoto wanahitaji mtu wa kuwasimamia katika baadhi ya mambo, kwa mfano watahitaji kuoa, sasa lazima baba zao wakubwa na wadogo wajue na washiriki.

“Huenda huko mbele wanaweza kuwa watu wa kunywa pombe kupita kiasi, nitawahitaji ndugu wa baba yao ili aweze kuwakemea, so hawa ni watu muhimu sana katika maisha yangu na watoto wa Ivan na sitarajii kugombana nao,” alisema Zari.

Credit - Global Publisher
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad