Breaking News: Huyu Hapa Atangazwa Kuwa Rais Mpya wa TFF....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli amemtangaza Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufuatia uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika leo Makao Makuu ya Tanzania Dodoma.


Wallace Karia ameibuka mshindi wa nafasi ya Urais wa shirikisho hilo huku nafasi ya Makamu ya Rais ikichukuliwa na Michael Wambura, kwa matokeo hayo Wallice Karia anakuwa mrithi wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Jamal Malinzi
Baada ya kutangazwa washindi viongozi hao waliweza kula kiapo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi, naa baada ya hapo Rais mpya wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF) Wallace Karia aliwashukuru wajumbe na watanzania kujumla na kusema kuwa furaha aliyonayo iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania.
Hata hivyo Wallace amesema katika uongozi wake uwazi na uwajibikaji ndiyo nguzo kuu na kusema hivi sasa ubabaishaji katika mpira wa miguu sasa umekwisha, ubabaishaji wa soka sasa ni mwisho.
Katika uchaguzi huo wajumbe wa Kamati Kuu ya Uchaguzi waliweza kuchagua pia Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) katika kanda mbalimbali mbao ni
Lameki Nyangaya (DSM)
Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga)
Francis Ndulane (Pwani na Morogoro)
Mohamed Adeo (Dodoma na Singida
Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara)
James Mhagama (Njombe na Ruvuma)
Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa)
Kenneth Pesambili (Rukwa na Katavi)
Issa Mrisho (Kigoma na Tabora)
Mbasha Matutu (Shinyanga & Simiyu)
Vedastus Lufano (Mara na Mwanza)
Salum Chama (Kagera na Geita)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad