Namna ya Kupunguza Tumbo Kubwa Au Kitambi.....

Katika jamii yetu wanawake ndio wanaohangaika zaid kutoa matumbo yao makubwa, utawasikia mara nyingi wakiulizia kuhusu dawa ya kupunguza tumbo kwa wanawake, lakini si kwa ajili ya kukwepa madhara ya kiafya, bali kwa ajili ya kuboresha mwonekano wao kiurembo-kwao ni suala la urembo tu na si suala la afya. Kwa upande mwingine akina baba huona fahari kuwa na vitambi, kwao kitambi ni dalili ya kunyookewa na maisha.

Katika mada ya leo tutazungumzia hayo matumbo makubwa na vitambi ambapo tutaona matumbo hayo au vitambi hivyo ni nini, tutaeleza madhara ya kuwa na matumbo hayo makubwa na mwisho kutoa ushauri wa jinsi ya kuyapunguza matumbo hayo.Nini Maana Ya Tumbo Kubwa Au Kitambi

Leo utasikia neno la ajabu kuwa “kila mtu ana kitambi, hata yule ambaye tumbo lake kwa nje linaonekana kuwa flat kabisa na kuwa kitambi kina madhara makubwa kwa afya yako kuliko aina nyingine yo yote ya mafuta yaliyo ndani ya mwili wako.”

Hii ina maana gani?

Kitambi ni mafuta na mafuta haya yanaweza kuwa chini ya ngozi yako au ndani kabisa kuzunguka moyo, mapafu, maini na viungo vingine. Ni mafuta haya ya ndani (visceral fat) ambayo yanaweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kiasi gani. Mwili huhitaji mafuta haya ya ndani kwa ajili ya kutenganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusuguana, lakini yakizidi huleta matatizo ya kiafya. Ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya high blood pressure, kisukari (Type 2 Diabetes), magonjwa ya moyo, kansa (kansa ya maziwa na kansa ya utumbo) na mengine. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo, na ndipo matatizo yanapoanza.

 Utapimaje Tumbo Lako?

 Kuna njia za kitaalamu za kupima kiasi cha mafuta ya ndani uliyo nayo ambazo ni CT Scan au MRI lakini pia unaweza kujipima mwenyewe ukapata picha nzuri tu ya hali yako. Chukua kipimo cha utepe, kile kinachotumiwa na mafundi cherehani (measuring tape), jipime eneo la kitovuni ukiwa umesimama huku ukihakikisha kuwa utepe ni mnyoofu. Kwa afya nzuri, kipimo kisizidi nchi 35 kwa mwanamke na kisidi nchi 40 kwa mwanamme.

Kuwa na mwili wenye umbo la pears “pear shape”, hips na mapaja makubwa, kunafikiriwa kuwa ni bora zaidi ya umbo la apple ambalo linamaanisha kiuno kipana zaidi. Kuwa na kiuno kipana kuna uwiano na kiasi cha mafuta ya ndani (visceral fat) uliyo nayo.


 Namna Ya kuondoa Matumbo

Tumeona hapo juu kuwa hata watu wembamba wana mafuta ya ndani ambayo yanaweza kuwasababishia matatizo ya kiafya. Uwingi wa mafuta unakuwa ni wa kiurithi, utalingana na style ya maisha unayoishi na jinsi gani mwili wako unafanya mazoezi – mafuta haya hupenda mtu asiyejishugulisha yaani yule ambaye anaufanya mwili wake kubweteka.

Maandiko mengi sana yameandikwa kuhusu namna ya kupunguza unene wa mwili na makampuni mengi yamekuja na dawa za kudai kupunguza unene wa mtu. Kimsingi ili mwili upungue unene, unahitaji kutumia kalori nyingi kuliko unazozipokea. Hili ni la kweli vilevile kwa mada yetu ya leo ya kupunguza tumbo kwani si rahisi kupunguza tumbo peke yake bila kupunguza sehemu nyingine za mwili. Ili kufanikisha azma ya kutumia kalori nyingi zaidi ya zile unazozipokea, hapa nashauri njia 4 za kuzitumia:1. Mazoezi Ya Viungo Ya Kupunguza Tumbo

Unaweza kufanya mazoezi ya aina nyingi ili kupunguza tumbo. Mazoezi yo yote ya nguvu yatapunguza mafuta ya mwili wako pamoja na mafuta ya ndani (visceral fat).

Mazoezi ya kadri ya dakika 30 mara tano kwa wiki yanafaa, kama vile kutembea, ili mradi unatoa jasho, yatakufanya uheme kwa haraka na kuongeza mapigo ya moyo wako.

Unaweza kupunguza muda kwa kufanya mazoezi ya nguvu zaidi kama jogging kwa dakika 20 mara nne kwa wiki.
 Unaweza kupata matokeo mazuri vile vile kwa kufanya mazoezi ya ndani ukiwa nyumbani mwako. Nitaonyesha video mbili katika ukurasa huu ili uweze kuchagua ile utayoiona kuwa inakufaa zaidi. Video hizi zinaonyesha mazoezi ambayo wengi wameyajaribu na kuona kuwa yaliwapunguzia matumbo yao katika muda mfupi. Cha msing ni kuanza na mazoezi mepesi na taratibu, kuongeza ugumu wake hadi kufikia mazoezi ya nguvu.

  
2. Chakula

Kuna maandishi mengi mno kuhusu somo hili la kupunguza mafuta ya mwili kwa kuwa na mpango mzuri wa ulaji chakula. Unaweza pia kusoma ukurasa wetu wa “Punguza Unene“. Kwa kifupi unahitaji kuzingatia yafuatayo:


  • Kula mboga za majani kwa wingi sana kulijaza tumbo lako
  • Kunywa maji mengi sana
  • Weka chakula cha kukutia hamu mbali na nyumba yako
  • Tafuta shughuli za kukufanya uwe busy kila wakati
  • Kula kutoka kwenye sahani tu ukiwa umeketi mezani
  • Kula milo yote, acha tabia ya kuruka milo3. Kupata Usingizi Wa Kutosha

Kupata usingizi kwa muda mzuri kumeonyesha kuwa na mchango katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika mwili wa binadamu. Katika utafiti mmoja, watu waliopata usingizi kwa saa 5 hadi 6 kwa siku katika kipindi cha miaka 5, walionyesha kuwa na mafuta mwilini kidogo zaidi ukilinganisha na wale waliopata usingizi kwa pungufu ya saa 5 kwa siku au wale waliolala kwa saa 8 au zaidi kwa siku.

4. Kuepusha Msongo Wa Mawazo

Kila mmoja wetu hapatwa na mawazo. Jinsi unavyoyachukulia mawazo hayo huwa na mchango mkubwa katika kujaza mafuta mwilini. Jaribu kushiriki katika mazungumzo na ndugu katika familia na marafiki zako. Mazoezi ndiyo ndiyo bora kabisa kwani hukutoa kwenye msongo wa mawazo wakati huo huo yakikupunguzia unene. Ukipungukiwa na mawazo utaweza kufanya maamuzi mazuri zaidi kuhusu maisha yako.

5. Kutumia Virutubishi

Kuna virutubishi ambavyo vimethibitika kusaidia kupunguza uzito wa mwili. Virutubishi vinafanya kazi vizuri ikiwa mwili utakuwa na kiwango kizuri cha madini ya calcium katika damu. Tafiti zimeonyesha kuwa asilimia moja ya madini ya calcium ndani ya mwili huwa katika mzunguko wa damu. Kiwango hiki cha calcium kikipungua, homoni ya parathyroid huzuia uvunjwaji wa mafuta katika mwili. Hivyo basi, kama kiwango cha calcium katika damu kitakuwa kimepungua, zoezi la kupunguza mafuta mwilini halitafanikiwa.

Baadhi ya virutubishi vya kupunguza mafuta mwilini ni kama:

1. Slimming Capsules2. Pro Slim Tea


 i.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Namna ya Kupunguza Tumbo Kubwa Au Kitambi..... Namna ya Kupunguza Tumbo Kubwa Au Kitambi..... Reviewed by Udaku Special on August 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.