9/28/2017

Meya Ubungo Aliamsha Dude Sakata la Bashite Apeleka Ushahidi Kwenye Kamati ya Maadili

Meya Ubungo Aliamsha Dude Sakata la Bashite Apeleka Ushahidi Kwenye Kamati ya Maadili
Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudaiwa kughushi vyeti vya elimu, limechukua sura moya baada ya Meya wa Ubungo, Boniphace Jackob, kutinga kwenye Kamati ya Maadili ya Watumishi wa Umma, ambako shauri alilolifungua dhidi ya mkuu huyo wa mkoa limesikilizwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kwenye kamati hiyo, Meya Jackob alisema ameitwa kuhojiwa masuala mbalimbali kuhusu shauri hilo, huku naye pia akidaiwa kukiuka sheria za utumishi wa umma kwa kufanya mkutano wa chama ndani ya ofisi za serikali ambapo amesema kwamba ameiambia kamati hoja yake ya msingi ni Paul Makonda kudaiwa kutumia vyeti vya mtu mwingine, wakati jina lake halisi ni Paul Albert Bashite.

Meya Jackob amesema anashukuru kwamba ushahidi wote alioupeleka kwenye kamati hiyo, umepokelewa na hakuna aliyejitokeza kuupinga hivyo anaamini mwisho ukweli utajulikana, huku akisisitiza kwamba yupo tayari kufanya kazi na Daudi Albert Bashite hata kama aliishia darasa la saba lakini anachotaka ni ukweli kufahamika.Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

  1. hapo meya umenena ni kweli kabisa tunataka kuona vyeti ilivo kuja kesi ya vyeti feki siku hizi hata muuza karanga lazima awe cmesoma itakuwa mkuu wa mkoa first of all he dont have personaĺitý ya cheo alicho pewa au ukabila umeanza he is bogus

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger