Ticker

6/recent/ticker-posts

Hudda Avutiwa Kutoka Kimapenzi na Jux Asema Yupo Single Hata na Mimi Ninapatikana

Hudda Avutiwa Kutoka Kimapenzi na Jux Asema Yupo Single Hata na Mimi Ninapatikana
Mwanamitindo na Mfanyabiashara kutoka Kenya, Huddah Monroe, amefunguka na kusema kwamba anadhanii Msanii Juma Jux wa Tanzania ni mwanaume ambaye yeye anaweza kuwa naye kimahusiano huku akimmwagia sifa kuwa anamuonekano mzurii kwenye mavazi.

Akifanya mahojiano maalumu na kipindi cha Nirvana kinachorusha kila Jumanne saa tatu usiku chini ya Mtangazaji Deogratius Kithama, Huddah alijibu swali la mtangazaji huyo kama anaweza kuwa kwenye mahusiano na Jux baada ya kumsifia kuwa ana muonekano wa tofauti na wenye kuvutia.
"Aaah, Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano...... Yupo 'single? hata mimi nitapatikana....." amesema Huddah
Aidha Huddah amemshauri Jux kufanya kolabo na wasanii wakubwa zaidi wa kimataifa ili azidi kuwa msanii kubwa zaidi ndani na nje ya kimataifa kwani anamuonekano wa kuwa mtu maarufu.
Mbali na hayo Huddah amekiri kwamba alishawahi kumcheki Jux kupitia mtandao na kumwambia jinsi gani anapenda muonekano wake wa mavazi na jinsi ambavyo anavaa tofauti na jinsi jamii zinavyomfikiria.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments