Hali si shwari Soka la Majirani Zetu Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hali si hali nchini Kenya, rais wa shirikisho la soka nchini humo Nick Mwendwa amesema kujiondoka kwa baadhi ya wadhamini waliokuwa wakidhamini shirikisho hilo pamoja na michezo ya ligi kuu kumelifanya soka la nchi hiyo kuanza kuyumba na wasiwasi umetanga kwamba huenda ligi ikasuasua lakini huenda timu ya taifa ikatetereka kwa sababu kama ligi haitochezwa kwa ushindani uliokusudiwa moja kwa moja timu ya taifa itaathirika.

Changamoto hiyo imekwenda mbali kidogo kwa sababu wadhamini wakubwa ambao walikuwa wakitoa kiasi kikubwa cha fedha katika soka la Kenya, kuondoka kwao pia kunaweza kufanya soka likadidimia.

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Nation David Kalimwa amezungumzia hali ya mchezo wa soka nchini Kenya baada ya kuondokewa na udhamini wa baadhi ya makampuni.

“Hali ya sintofahamu imelikumba soka la Kenya baada ya kuondokewa na wadhamini wakubwa Sport Pesa kujiondoa katika udhamini pamoja na mashirika mbalimbali ikiwamo vilabu vikuu hapa nchini Kenya AFC Leopard na Gor Mahia pamoja na klabu ya daraja la pili Nakuru All Stars na shirikisho la soka la Kenya Football Kenya Federation (FKF) na wasimamizi wa ligi kuu ya Kenya ambao wote walikuwa wananufaika kwa udhamini wa takribani dola milioni sita za Marekani kwa mwaka sawa na shilingi milioni 600 za Kenya.”

“Sport Pesa wamejiondoka kwenye udhamini kwa sababu serikali ya Kenya imeongeza kodi kwa makampuni yote ya betting, kujitoa kwa Sport Pesa kumeleta shida mbalimbali ambapo wasimamizi wengi wa soka hapa nchini wamesema labda hakuta kuwa na maendeleo ya michezo lakini rais wa FKF Nick Mwendwa ambaye alidai wanafanya mazungumzo na serikali kuona kama itaweza kudhamini michezo hiyo ya ligi bada ya Sport Pesa kujiondoa.”

“Kampuni ya Sport Pesa pia ilikuwa ikilipa mshahara wa kocha mkuu wa Kenya pamoja na mkurugenzi wa ufundi wa FKF kwa hiyo kujiondoa kwa Sport Pesa kunaweza kufanya wawili hao kukosa mishahara.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad