Aliyejiuzulu Bavicha: Mimi Bado Mwanasiasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyejiuzulu Bavicha: Mimi Bado Mwanasiasa
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Gertrude Ndibalema amesema licha ya kujiuzulu wadhifa huo, hana mpango wa kuachana na siasa.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Machi 13, 2018  amesema siasa ni maisha na ni ngumu kwake kama kijana kuachana nayo, “nisiposikika katika ulingo huo wa siasa nitaonekana tu. Siwezi kufanya uamuzi wa ajabu kama huo wa kuacha siasa, nimejiuzulu nafasi hiyo, lakini mimi bado ni mwanasiasa ukizingatia umri unaniruhusu.”

Amesema katika nafasi ya uongozi aliyokuwa nayo changamoto zilikuwa nyingi, lakini alikuwa anatoa ushauri kwa viongozi wa chama na kwamba zipo zilizofanyiwa kazi na ambazo hazijafanyiwa kazi.

Kuhusu demokrasia nchini amesema, “Nchi ili iwe na  demokrasia lazima iwe na siasa safi na uongozi bora, swali la kujiuliza ni kwamba Tanzania kuna vitu hivyo viwili.”

“Kama hakuna vitu hivyo ina maana bado hatuna demokrasia, kuna kukatazwa mikutano ya siasa, kukatazwa maandamano, kuna vitu vichache vikifanyiwa kazi kila kitu kitakuwa sawa.”

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 alitangaza kujiuzulu Machi 12, 2018 kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad