13 Mar 2018

Baraza la Wazee wa Chadema Laomba Kukutana na Rais Magufuli

Baraza la Wazee wa Chadema Laomba Kukutana na Rais Magufuli
Baraza la Wazee wa Chadema limemuomba Rais John Magufuli kukutana na  wazee ili kubadilishana nao mawazo sambamba na kumpa ushauri wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Akizungumza leo Jumanne Machi 13, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema kumekuwa na mambo mengi yanayopigiwa kelele, ni vyema rais akakutana na wazee ili wamueleza mambo hayo.

“Ni lazima kama Taifa tuchukue hatua mapema kabla hatujachelewa. Rais Magufuli akubali kuitikia wito wa kukutana na wazee ambao watakuwa na ujasiri wa kumshauri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye majanga,” amesema.

Amesema suala la wazee kukutana na rais, kimekuwa ni kilio cha muda mrefu na kwamba nchini Kenya viongozi wameweza kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao.

“Lazima tukae tujue mustakabali wa Taifa hatuwezi kusema hakuna tatizo. Tunamtaka akutane na wazee, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa tuzungumze kwa kuwa hii ni nchi yetu wote na si ya chama kimoja,” amesema.

Amesema mambo yanayopaswa kuzungumziwa ni suala la Katiba Mpya, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Amesema pia matukio ya watu kutekwa na kuuawa yameongezeka, “miezi sita iliyopita tulizungumzia mambo haya lakini naona ndio yanaongezeka.”

“Wazee tumeuziwa mno kuhusu suala la Abdul Nondo hasa pale Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu Nchemba) alipotoa kauli kuwa kijana huyu alijiteka. Tulitegemea polisi wafanye uchunguzi, sasa kama waziri mhusika tayari ameshatoa hukumu tutegemee nini kwa hawa polisi. Tunajenga nini ndani ya mioyo ya hawa vijana ambao walijitoa kumtetea kijana mwenzao kama si chuki.”


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

  1. Magufuli asije kupoteza wakati wake au hata kufikiria kukatana na hawa wanaojiita wazee wa Chadema. Hawahawa ndio wenye kushiriki na kupanga mikakati ya kuichafua nchi halafu leo wanajifanya wanataka kuonana na Raisi? Magufuli kama kusoma basi ajifunze kwa tukio la Edward Lowasa. Magufuli alimpokea Lowasa kwa nia nzuri kabisa matokeo wanasema alimuita kwenda kumbembeza arudi CCM. Magufuli ambembeleze fisadi? Lakini Chadema wote walinuna kwanini Lowasa kaenda kuonana na Magufuli? Halafu leo hawa wanaojiita wazee wa Chadema wanajifanya kutaka kuonana na Raisi Magufuli kutafuta Amani tena? Tanzania ni nchi ya Amani tena sana mpaka hivi sasa tunavyozungumza isipokuwa kuna baadhi ya watu wanaojiita wanasiasa wa upinzani wanaongozwa na Chadema, kwa makusudi kabisa wameamua kumpiga vita Magufuli tangu day one alupoapishwa kuwa Raisi wa nchi hii. Katika harakati hizo za kumpiga vita Magufuli wamejaribu kila aina ya maigizo kuipaka matope serikali ya Magufuli ili ionekane hakuna anachokifanya. Lakini watu hao wenye nia chafu baada ya kuona Magufuli hatingishiki na upuuzi wao sasa wanaamua kuwashawishi watu kufanya vurugu kwa kisingizio cha demokrasia. Huyuhuyu mtu aliejitokeza kuwa msemaji sijui kiongozi wa baraza la wazee wa Chadema ndie aliekwenda kumtetea yule mwanafunzi aliejiteka na kama vile haitoshi mzee huyo akamwagia maneno ya shombo waziri wa Mambo ndani, yaani anakwenda kuingilia kazi za kipolisi kabla hata hawajakamilisha kazi yao. Sasa wazee waliokosa busara kupitiliza mipaka kiasi hicho wanakwenda kuonana raisi kumueleza nini? Kabla ya yote huyu mzee anatakiwa kumuomba radhi waziri wa mambo ya ndani kwa kitendo chake cha kumshutumu kuwa alikuwa na nia ya kutaka kumnyima haki yake yule Mwanafunzi aliejiteka . Mkutano wa kweli unaotakiwa kufanywa Tanzania ni mkutano kati ya Chadema na washirika wake wanaohubiria nchi haina amani kiasi cha kuonesha wazi kwamba wakifurahia hayo matamshi yenye kuashiria vurugu. wajiulize wao wenyewe nini wanachokitaka kitokee katika nchi hii kwani inaonekana kama wamechanganyikiwa na kutaka kuwachanganya watanzania waliowengi na chonde chonde....wamuache Raisi aendelee kuchapa kazi. Ila anatakiwa kuajiri watu wa usalama wa taifa wa kutosha zaidi na waliofundika vyema. Wenye uwezo wa kunusa harufu yeyote mbaya ya kiuhalifu mapema zaidi kabla jambo kutokea.

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger