Dawa Zinaniponza Mimi Naziacha- Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dawa Zinaniponza Mimi na Naziacha- Wema Sepetu
Mkurugenzi wa kampuni ya Endless Fame, Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa dawa ambazo anatumia ndiyo zinamponza kuwa na mwili mkubwa ambao yeye mwenyewe haupendi na kusema kuwa kwa sasa anatamani kuziacha ili aweze kupungua mwili wake.


Wema Sepetu ameweka wazi hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Instgram wakati akimjibu msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Ray C ambaye ameweza kufanikiwa kupunguza mwili wake na kilo na kurudi kwenye ubora wake kama zamani. Ray C alikuwa akiwakumbusha Shilole pamoja na Wema Sepetu kuwa wanaweza kupunguza miili yao na kilo na kuwa kama zamani kwa kujitolea mfano yeye.

Kufuatia kauli hiyo ya Ray C ndipo mwanadada Wema Sepetu alipoamua kuweka wazi kuwa si mapenzi yake yeye kuwa na mwili huo alionao sasa bali ni kutokana na matumizi ya dawa, ambazo hakuweka wazi ni dawa zipi, ingawa baadhi ya mashabiki wameunganisha na kudai kuwa huenda msanii huyo anatumia dawa zitakazomsaidia ili aweze kuja kushika ujauzito, huku wengine wakisema ni matumizi ya dawa za kupunguza mwili.

"Yaani mimi sielewi jamani siyo mimi dada yangu...Dawa zinaniponza mimi na naziacha" aliandika Wema Sepetu

Baada ya jibu hilo Ray C alirudi tena na kumpa pole Wema Sepetu na kumweleza kuwa hakuna namna tena inabidi azikate ili aweze kupungua na kudai kuwa inawezekana kabisaa Wema Sepetu akarudi kama zamani endapo atazingatia mafunzo, mpangilio mzuri wa chakula na kusema kabla ya mwaka atampa matokeo ya hilo.

"Pole wangu inabidi uzikatie tu hakuna namna, inawezekana kabisa yaani niamini mimi !a good trainer! proper diet! less than a year utaniambia! uamuzi tu, najua unaweza Wema Sepetu" alisema Ray C
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizo dawa anazotumia Wema itakuwa ni bangi ambayo alikutwa nazo pia ana kesi nayo sababu bangi inakufanya mtu ule sana kwa wanaume hawawezi kuongezeka mwili sababu wanafanya sana kazi sasa kwa wanawake ambao wanakaa tu bila kufanya kazi yeyote ndiyo hivyo mwili unaongezeka

    ReplyDelete

Top Post Ad