Lema Amzungumzia Nguvu Aliyonayo Mange Kimambi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lema Amzungumzia Nguvu Aliyonayo Mange Kimambi
Mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA Mhe, Godbless Lema amefunguka na kuweka wazi kuwa kama chama cha siasa hakiwezi kufundisha watu wake kufanya siasa za kuleta fujo bali uvunjifu wa amani, uonevu ni vitu ambavyo vinaweza kuwafanya watu wapiganie haki zao


Lema amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya CHADEMA na kusema kuwa wapo watu wengi ndani ya CHADEMA na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakilia na kuumia na mambo yanayoendelea nchini ndiyo maaana hata mwanaharakati Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii amekuwa na nguvu kwa kuwa kuna watu ambao wanasikiliza kutokana na mambo yanayofanywa na serikali.

"Yaani msingi wa kwanza wa Demokrasia ni amani maanake watu washindane kwa hoja sasa inatosha maanake nini kumekuwepo na vilio vya CHADEMA na wanachama wake kwa muda mrefu sana bahati mbaya waandishi wa habari mkafikiri vilio hivi vya CHADEMA, kanisa likafikiri hivyo na msikiti ukafikiri hivyo lakini leo tunalia pamoja wakiwepo wafanyabiashara sasa leo kilio chetu si pekee yetu ndiyo maana kanisa limetoa waraka hivi karibuni Katoliki na Lutherani tunategemea BAKWATA watafanya hivyo hivyo sasa ipo siku na hiyo siku inakuja"

Lema aliendelea kusema kuwa "Kuna uchungu unakusanyika kwa watu na hawa watu wanaandamana moyoni ndiyo maana Mange Kimambo yuko Marekani anatumia Instgram huku anajibiwa na kiongozi, Mwigulu Nchemba, Mambosasa, sasa kama mtu mmoja yupo Marekani anaweza kuhamasisha Tanzania na kukawa na presure tunayoiona hii manake kwamba watu wamechoka, tunasema imetosha lengo la CHADEMA au lengo langu mimi au lengo la kiongozi yoyote wa CHADEMA si kuona nchi hii haina amani lakini lengo la Chama Cha Mapinduzi kwa mwelekeo wao ni kuona watu wanaingia barabarani kwa nguvu kutafuta haki" alisema Lema
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mfyuuuu! Usisema watu wamechoka, sema wewe na chadema yako mmechoka kisiasa...anzisheni timu ya mpira wa pete sasa..... huyo mange wenu kama ni mwanamke anayejiamini hasa, hebu alete 'ngoko' zake huku TZ aongoze hayo maandamano...amekuwa kama 'mmbu' nje ya chandarua, makelele meeengii lakufanya HANA...hebu jaribuni kuitisha hayo maandamano tuone....KILA-MCHUMA-JANGA-ULA-NA-WAKWAO.....mtajutraaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad