Timotheo Wandiba Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 81

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Timotheo Wandiba  Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 81
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imemuhukumu miaka 81 jela mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujipatia fedha ambazo ni Sh.Bilioni 2.1 kwa njia ya udanganyifu.

Mbali ya Wandiba, pia mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wenzake wawili ambao ni Dickson Okololo na Simon Efrem ambao hawakutiwa hatiani.

Akisoma hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu Joyce Minde, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82, ambapo Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 14.

Katika makosa hayo 82, mashtaka 27 ni ya kughushi, 27 ya kutoa hati za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na Moja la utakatishaji fedha.

Hakimu Mashauri amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa Wandiba katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka.

“Katika makosa hayo 27 kwa kila kosa unahukumiwa kwenda jela miaka 3 ambapo jumla itakuwa ni miaka 81 lakini adhabu hiyo utataumikia sambamba,” -Hakimu Mashauri.

Pia Hakimu Mashauri amesema mahakama hiyo imemuachia huru Wandiba na wenzake, Okololo na Efrem katika makosa mengine yote.

“Pia mahakama inawaachia huru mshtakiwa Okololo na Efrem katika mashtaka yote na Wandiba katika mashtaka ambayo hakutiwa hatiani,”. -Hakimu Mashauri.

Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ikiwemo kughushi, utakatishaji fedha na uwasilishaji wa nyaraka za uongo.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambalo limemtia hatiani Wandiba, inadaiwa kati ya December 3,2012 na February 5,2013 katika jiji la Dar as Salaam alijipatia Sh.Bilioni 2.1 kutoka Benki ya Africa (BoA) kwa njia ya udanganyifu.

Pia katika makosa ya kughushi inadaiwa walilitenda February 3,2012 na January 31,2013 jijini Dar es Salaam ambapo walighushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha kutoka Benki ya BoA ikionyesha akaunti ya Sogea Sauthom imeiomba benki hiyo kuilipa akaunti ya Tracom Sh.Bilioni 2.1.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya December 4,2012 na April 30, 2014 ambapo walijipatia Sh.Bilioni 2.119,039,398.96 kutoka akaunti ya Sogea Sauthom katika benki ya (BoA) kwenda akaunti ya Tracom NMB tawi la Ban House wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu la kosa la kughushi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo akanye katika debe miaka 81 kama ataishi hiyo miaka 81

    ReplyDelete

Top Post Ad