Hivi Ndivyo Lulu Alivyosheherekea Birthday Akiwa Gerezani ....Atoa Zawadi kwa Watoto Wanaopatiwa Matibabu Muhimbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hivi Ndivyo Lulu Alivyosheherekea Birthday Akiwa Gerezani ....Atoa Zawadi kwa Watoto Wanaopatiwa Matibabu Muhimbili
April 16 kama ya leo miaka kadhaa iliyopita alizaliwa Elizabeth ‘Lulu’ Michael ambaye kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka miwili.



Katika kusherehekea siku hii, mrembo huyo ameamua kutoa zawadi kwa watoto ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili.

Zawadi hizo ziliwakilishwa na mama yake mzazi pamoja na msanii mwenzake wa karibu zaidi Dokta Cheni. Lulu pia ametoa ujumbe wa kuwafariji wagonjwa hao pamaoja na wazazi wao.

Ujumbe huo ambao ulisomwa kwa niaba na Dokta Cheni umesema, “Nawapenda sana watoto na nawaombea kwa Mungu. Naamini wakiwa huru kumuomba Mungu na wao wazazi hayo maradhi yanayowakabili yatapona kwa muda mfupi. Ninawatakia kila la kheri na muweze kupona haraka.”



Hii ni mara ya pili kwa Lulu kuchangia katika shughuli za kijamii huku mwenyewe akiwa gerezani, mwezi uliopita alichangia pedi kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kupitia kampeni iliyokuwa inaendeshwa na kituo cha runinga cha EATV na Msichana Initiative.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad