5/22/2018

Mama Diamond Asota Polisi kwa Masaa Sita Kisa Hiki Hapa

Mama Diamond Asota Polisi kwa Masaa Sita Kisa Hiki Hapa
UCHUNGU wa mwana aujuaye mama! Hicho ndicho kilichotokea kwa mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sandra Kassim a.k.a Bi Sandra ambaye alifikia uamuzi wa kusota Polisi kwa saa 6, kisa mwanaye, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.Mama huyo alijikuta akihenya wikiendi iliyopita katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama a.k.a Mabatini jijini akijaribu kumnasua Esma baada ya kutiwa mbaroni baada ya kunaswa na wakaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akiuza vipodozi vilivyopigwa marufuku.


Habari zilieleza kuwa, Esma alikutwa akiuza vipodozi hivyo vyenye kemikali kwenye saluni yake iliyopo Sinza, Afrika Sana jijini Dar.

Kwa mujibu wa habari za kishushushu ndani ya kituo hicho, katika sakata hilo, maofisa hao walikuwa kwenye msako wa operesheni maalum wa wafanyabiashara wanaoendelea kuuza vipodozi hivyo.Taarifa hizo zilieleza kuwa, Esma alikamatwa na wakaguzi hao majira ya saa 9:00 jioni ambapo baada ya taarifa hizo kumfikia mama Diamond alifika kituoni hapo akiambatana na watu wengine akiwemo, babamkwe wake, Petit Man ambaye ni mume wa Esma.

Mama Diamond, akiwa na kampani yake, walijaribu kumchomoa Esma mahabusu kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa 6:00 usiku, lakini ngoma ilikuwa ngumu.Ilielezwa kuwa, maafande wa Mabatini walikuwa hawaingiliki, hali iliyosababisha malumbano ambapo Ijumaa Wikienda, likiwa kituoni hapo lilimshuhudia Mama Diamond akilumbana na maafande hao baada ya kila alilowaeleza ili wamuachie mwanaye kushindikana.“Hapa leo hatoki mtu, hata umuite Diamond, sisi hatuwezi kumuachia mwanao mpaka tupewe amri na maofisa wa TFDA waliomkamata,” alisikika mmoja wa maafande hao huku akikataza watu kusogelea kituoni hapo hasa baada ya giza kuingia.


Baada ya mama Diamond kutimuliwa eneo hilo usiku huo, asubuhi yake, Ijumaa Wikienda lilidamkia tena kituoni hapo na kumkuta mama huyo akiendelea kuhaha kumnasua Esma ambaye usiku wa kuamkia Jumamosi alilala korokoroni.Hadi Ijumaa Wikienda linang’oa nanga kituoni hapo mchana wa Jumamosi iliyopita, bado Esma alikuwa akiendelea kushikiliwa mahabusu kwa kosa hilo ambapo alifunguliwa kesi kwenye jalada namba KJM/RB/4427/2018 kwa kosa la KUKUTWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

4 comments:

 1. bado malipo mengine yanakuja. wa kwake anauma ila wa mwenzake alimdhalilisha mpaka kwenye mitandao. bitch..

  ReplyDelete
 2. Karma mbona haitangazi? alijiona mbabe kwa mtoto wa mwenzie. tulia mlezi wa viben ten. Mengine yako njiani.

  ReplyDelete
 3. kiki za mama d bwana mtu mzima ovyo

  ReplyDelete
 4. jitu zimaaa, halijiheshimu kutwa anatafuta kiki. enzi zake alikuwa anajiuza Magoti hasemi.

  ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger