13 Jun 2018

Hispania Yamtimua Kocha Wake, Siku Moja Kabla ya Kombe la Dunia

Hispania Yamtimua Kocha Wake, Siku Moja Kabla ya Kombe la Dunia
Chama cha soka nchini Hispania kimemtimua kocha wake, Julen Lopetegui hii leo ikiwa imesalia siku moja pekee kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 51 ameondolewa kwenye nafasi hiyo mara baada ya kutangazwa na klabu ya Real Madrid kuchukua mikoba ya
Zinedine Zidane aliyeachana na kibarua cha kuendelea kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wa klabu bingwa barani Ulaya.

Rais wa chama hicho chenye dhamana ya kusimamia mchezo wa soka Hispania, Luis Rubiales alitangaza kuachana na kocha huyo na kumtakia kila lakheri kwenye majukumu yake mapya.

Rubiales amesema kuwa mazungumzo ya Lopetegui na Madrid yamefanyika pasipo kushirikisha chama hicho na kuelezwa dakika tano kabla ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger