google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Selikali Kumchukulia Hatua Kali Mwalimu wa Mt Florence Anayewanajisi Wanafunzi | UDAKU SPECIAL

Selikali Kumchukulia Hatua Kali Mwalimu wa Mt Florence Anayewanajisi Wanafunzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Selikali Kumchukulia Hatua Kali Mwalimu wa Mt Florence Anayewanajisi Wanafunzi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako Ndalichako ameweka wazi kwamba serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya udhalilishaji  ambavyo vimeonekana kufanywa na mwalimu wa shule St. Florence iliyopo jijini Dar es salaam.


Waziri Ndalichakoameyasema hayo  wakati akikabidhi zawadi kwa shule na wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na sita jijini Dodoma  baada ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mwisho ya mitihani yao.

Akizungumzia suala hilo Ndalichako amewahakikishia wananchi kuwa mwalimu aliyewafanyia udhalilishaji wanafunzi wa kike wa shule ya Mt. Florence vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi lakini watahakikisha serikali inawamchukulia hatua kali.

Pamoja na hayo Waziri Ndalichako ameshauri walimu wa kike kusafiri na wanafunzi wa jinsia ya kike katika ziara mbalimbali za kishule badala ya wanaume ili kuepukana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kama ilivyowatokea wanafunzi wa shule St. Florence.

Hivi karibuni kuliibuka sintofahamu ndani ya jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla baada ya kuwepo na taarifa kwamba katika shule ya St. Florence mwalimu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ayubu kudaiwa kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba.

Hata hivyo tukio hilo bado lipo chini ya vyombo vya sheria linafanyiwa uchunguzi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad