Amber Lulu Amuomba Daimond Kumsajili WCB "Mzee wa Vikuku si Niwe Msanii Wako au Unasubiri Uvae Kikuku cha Pili"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni kweli Amber Lulu anahitaji kusaidiwa na label ya WCB ya Diamond au alimua kumpiga dogo muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo, Baila.


Muimbaji huyo ametumia picha ya Diamond iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii tangu juzi kama fursa ya kumwaga ombi lake hadharani ili limfikie Bosi huyo wa WCB.

Juzi, Diamond alizua tafrani mitandaoni alipoweka kipande cha video kinachomuonesha akiwa anapiga kazi jukwaani nchini Marekani lakini mguuni amevaa cheni, mtindo ambao ni maarufu kwa wakaazi wa Pwani kama Kikuku, na mara nyingi huvaliwa na warembo.


Hata hivyo, Diamond alikazia zaidi kwa kupost picha nyingine ikimuonesha ametulia baada ya kazi lakini ‘kikuku’ kilionekana kwa ukaribu zaidi mguuni kwake. Huenda Mkali huyo wa Baila alitumia mazingira sahihi kufanya kile ambacho ni kawaida kwa Wamarekani aliokuwa anawapigia show, lakini tafrani nyumbani. Wasanii kama Fabolous na wengine wamekuwa wakivaa Kikuku mara kwa mara wanapokuwa jukwaani.

Amber Lulu alitumia picha hiyo kumuomba Diamond kumpa nafasi ya kuwa Bosi wake na kumuomba ampe mkataba wa kuwa mmoja kati ya wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Hakika alijua picha hiyo maarufu itabeba ujumbe wake na kuufikisha mbali.

“Sema mzee wa vikuku, si niwe tu msanii wako jamani kwani unasubiri mpaka uvae kikuku cha pili @diamondplatnumz,” ameandika Amber Lulu.

Amber Lulu ambaye wimbo wake ‘Jini Kisirani’ ulipata mafanikio makubwa zaidi katika muziki wake ukitazamwa zaidi ya mara 2,000,000 kwenye YouTube, sio msanii pekee mwenye kiu ya kujiunga na lebo ya WCB.

Related Articles
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad