Kisa Kikuku Alichovaa Diamond, Vanessa Mdee Ampiga Mkwara Mkali Jux

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ameweka wazi kuwa amemchimba mkwara mzito mpenzi wake Jux kuhusiana na kuvaa kikuku.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Vanessa amefunguka kuwa uvaaji wa vikuku sio utamaduni wa wanaume wa Kitanzania hivyo hawezi pendezwa na utamaduni huo kwa madai umamshushia heshima mwanaume.

Kusema kweli Jux hawezi kuvaa kikuku  Sidhani kama inaendana na tamaduni zetu. Vikuku ni kwaajili ya wasichana, sipendi japo naona kuna watu wengi wanavaa”.

Vanessa aliongeza kuwa;

Kiukweli kuna msanii wa Marekani anampenda Jux anaitwa Fabulous, na yeye nahisi anavaa kikuku, nikasema nini hiki, nikamwambia ole wako na wewe uvae”.

Siku chache zilizopita Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa amevaa kikuku Kwenye mguu jambo ambalo watu wengi halikuwavutia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad