7/09/2018

Kocha wa Hispania Ajiuzulu Baada ya Kuondolewa Kombe la Dunia

Kocha wa Hispania Ajiuzulu Baada ya Kuondolewa Kombe la Dunia
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Hispania, Fernando Hierro (50) ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuondoshwa katika michuano ya Fainali za Kombe la Dunia 2018, zinazoendelea nchini Urusi.Hierro amefikia uamuzi huo ikiwa ni ikiwa hata mwezi mmoja haujatimia tangu Juni 13, 2018 alipoteuliwa kuwa kocha wa muda baada ya kocha wa taifa hilo Julen Lopetegui kufutwa kazi siku m oja kabla ya kuanza michuano hiyo kufuatia kutangazwa kwake kuwa Kocha wa Klabu ya Real Madrid.Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Uhispania, Hierro ambaye ambaye aliwahi kuichezea Madrid amekataa kurejelea katika wadhifa wake wa wa zamani wa mkurugenzi wa michezo, badala yake ameamua kutafuta mambo mengine ya kufanya.


Hata hivyo, Hispania ambao ni mabingwa hao wa Kombe la Dunia wa mwaka 2010 waliondolewa kwenye michuano hiyo kupitia mikwaju ya penalti na wenyeji Urusi hatua ya 16 bora.Lopetegui aliteuliwa kuwa Kocha wa Hispania mwaka 2016 baada ya kustaafu kwa Vicente del Bosque na alikuwa hajashindwa hata mechi moja kufikia wakati wa kuondoka kwake. Alifutwa kazi siku mbili kabla ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Ureno baada yake kutangazwa kuwa Kocha mpya wa Real Madrid, wadhifa uliobaki wazi baada ya kujiuzulu kwa Zinedine Zidane.Uhispania waliongoza Kundi B chini ya Hierro katika Kombe la Dunia. Hata hivyo, walikuwa wametoka sare ya 3-3 dhidi ya Ureno baada ya kufungwa dakika za mwisho, na walikuwa nyuma 2-1 dhidi ya Morocco kabla ya kusawazisha dakika za mwisho.Baada ya kutupwa nje kwao Urusi, Hierro alisema aliamua kuwajibika kutokana na kushindwa kwao kusonga.

“Tulijitolea kadiri ya uwezo wetu lakini hii ni soka, sifikiri unaweza kuzungumzia kuhusu timu kusambaratika au kuporomoka. Kuna mstari mwembamba sana kati ya kushinda na kushindwa,” alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger