Lugola "Sitaki Kuona Wafungwa Wanakula Bure Bila Kufanya Kazi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


DAR: Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewekea msisitizo kauli ya Rais Magufuli kuhusu wafungwa akisema hataki kuona wafungwa wanaishi kama ndege wa angani, akimaanisha kuwa wanakula bure bila kufanya kazi

Amesema Wafungwa wanatakiwa wafanye kazi na kujitafutia chakula wao wenyewe badala ya kusubiri kupewa chakula na Serikali

Amesema “Hata kama ni meno, lazima walimie meno, watatumia meno yao kulima mahindi, kulima maharage ili wajilishe, na nimemwambia Inspekta Jenerali wa Magereza, katika hili sitaki kisingizio cha aina yoyote"

Aidha, amewaagiza wasaidizi wake kupitia sheria vizuri na kumpelekea mpango mzuri wa kuwatumia wafungwa kufanya kazi za kilimo na ufugaji na kujitafutia chakula wao wenyewe

Ameongeza kuwa utoaji wa chakula bure gerezani umepelekea baadhi ya wafungwa kuona gerezani kama ndiyo sehemu ya kupumzika na kula bure bila kufanya kazi, hivyo hufanya makosa ya makusudi ili kurudi gerezani
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad