Mainda Adai Mitandao Imeharibu Msiba wa Patrick

Mainda  Adai Mitandao Imeharibu Msiba wa Patrick
MKONGWE kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kwa uchungu kuwa, kama sio timu za kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram, mtoto wa muigizaji Rose Alphonce ‘Muna’, Patrick angezikwa vizuri bila kutokea figisu zilizotokea.

Akizungumza hivi karibuni akiwa msibani Mwananyamala-Kisiwani jijini Dar, Mainda alisema anaamini watu wa mitandaoni wamechangia kwa kiasi kikubwa kuweka taarifa za upotoshaji kati ya Muna na mumewe Peter ambazo zimesababisha wawili hao washindwe kuelewana haraka.


“Jamani hivi ni vitu gani? Ndiyo maana mimi sipo kwenye mitandao nina sababu kubwa sana. Kuna upotoshaji wa hali ya juu na kama isingekuwa mambo ya matimu haya kusingetokea mvutano mkubwa uliokuwepo na kusababisha mambo mazito kwenye msiba wa mtoto asiyekuwa na hatia kabisa,” alisema Mainda huku akilia.


Mwili wa Patrick ulipumzishwa katika makazi yake ya milele juzi Jumamosi kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mainda Adai Mitandao Imeharibu Msiba wa Patrick Mainda  Adai Mitandao Imeharibu Msiba wa Patrick Reviewed by Udaku Special on July 09, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.