Yanga Yajipanga Kupambana na Gor Mahia Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Yajipanga Kupambana na Gor Mahia Kesho
Kikosi cha Yanga kinafanya maandalizi ya mwisho leo kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa kesho jijini Nairobi, Kenya.

Yanga inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu za kwenda suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ambayo wapo nayo kundi moja (Kundi D), mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi ya keshio itawapasa Yanga kuhakikisha wanapata ushindi kujiwekea mazingira ya kusalia kwenye michuano hiyo ambapo hivi sasa bado wana alama moja pekee katika msimamo wa kundi hilo.

Ikumbukwe Yanga ilipoteza dhidi ya MC Alger kwenye kibarua cha kwanza pia suluhu dhidi ya Rayon na kuwafanya kuwa kwenye mazingira magumu kunako kundi D.

Dawa pekee ya Yanga kujipa matumanini ni kuhakikisha inawafunga Gor Mahia kesho kisha kuanza maandalizi mengine ya mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani bila wachezaji wake mabeki Hassan Kessy na Yondani ambao imeelezwa wamebaki Dar es Salaam wakihitaji kuongezewa mikataba mipya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad