Dkt. Bashiru Awashika Koo Wanaotaka Urais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ali amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho, kufuta ndoto walizokuwa nazo za kutaka kushika madaraka ya urais wa Zanzibar licha ya kuwa muhusika yupo na muda wake haujakwisha kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM huko visiwani Zanzibar katika ziara yake ya kazi baada ya kusikia tetesi, kuwa kuna baadhi ya viongozi wa CCM wameanza kuunda makundi yenye lengo la kutaka kumtoa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.

"Wapo watu nasikia wengine wana vyeo na wengine hawana, wana ndoto ya kushika madaraka ya urais wa Zanzibar hiyo nafasi haijatangazwa kuwa wazi bado ina mwenyewe. CCM sio chama cha kusaka vyeo ni chama cha mapinduzi, wafuata vyeo 'wakome'. Tutaendelea kuwafuatilia wengine tunawajua na siku zenu zinahesabiwa. Muacheni Rais Shein amalize kipindi chake kwa heshima. Wakazi ukifika tutasema na kuweka utaratibu", amesema Dkt. Bashiru.

Pamoja na hayo, Dkt. Bashiru ameendelea kwa kusema "kiongozi mzuri haundi makundi kutafuta cheo, bali anasubiri kuombwa na watu kwasababu wanaomuomba ndio wanaomjua. "Wewe hujijui na wapo wengine ukiangalia orodha hata ukimpa ukuu wa wilaya hauwezi halafu anataka kuutafauta urais".

Aidha, Dkt. Bashiru amebainisha kwamba endapo nafasi hiyo ya urais itakuwa wazi basi wataitangaza kwa mujibu wa sheria kufuatana na chama chao kinavyosema na sio kupitia makundi ya watu yanayoendelea mahotelini.

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa tokea alipoteuliwa mnamo Mei 29, 2018, hii ndio ziara yake ya kwanza kufika visiwani Zanzibar na kutoa kauli kama hizo kwa watu wenye lengo la kutaka kushika nyadhfa za urais bila ya kufuata sheria isemavyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad