Hatimaye Mzee Majuto Kuzikwa Leo Tanga

Hatimaye Mzee Majuto Kuzikwa Leo Tanga
Mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani 'Mzee Majuto' umewasili Donge nyumbani kwake  jana 7.05 usiku . Safari ya kwenda Tanga kwaajili ya mazishi ilianza saa 10.15 jioni baada ya kumuaga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Leo  Agosti 10, kuanzia saa 5.45 mchana, ibada ya mazishi itafanyika katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake na kuzikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo cha jiji la Tanga.

Mzee Majuto alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Tezi Dume ambapo Januari mwaka huu,alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kupelekwa India kwa Matibabu zaidi . June 23, mwaka huu  alirejea nchini na kupelekwa moja kwa moja  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Hatimaye Mzee Majuto Kuzikwa Leo Tanga Hatimaye Mzee Majuto Kuzikwa Leo Tanga Reviewed by Udaku Special on August 10, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.