10 Aug 2018

Kalanga Aivuruga CCM Monduli, Wengine Wakimbilia Chadema


Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Monduli lililopo mkoani Arusha wanaompinga mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo hilo aliyepitishwa na chama hicho, Julius Kalanga wameapa kumuunga mkono mtoto wa Lowassa.

Aidha, habari kutoka Monduli zinasema kuwa baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameweka wazi kuwa watamuunga mkono mtoto wa Lowassa kwa madai kuwa utaratibu wa kumteua Kalanga umekiukwa.

Kalanga alichukua na kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo akiwa mwanaCCM pekee ambaye anatarajia kuchuana vikali na mgombea kutoka Chadema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Monduli, Wilson Lengima amesema kuwa hadi siku ya mwisho ya kuchukua fomu za ubunge ni Kalanga peke yake aliyekuwa amechukua.

Hata hivyo, mapema wiki hii kundi la wanachama wa CCM zaidi ya 40 kutoka kata tatu kati ya 20 za wilaya ya Monduli waliandamana kumpinga Kalanga kugombea ubunge kupitia chama hicho na kutuhumu kuwa kuna njama za kumfanya mgombea pekee.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger