Kipigo cha Polisi Chaharibu Figo ya Bobi Wine..Madaktari Wajitolea Kumtibu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Kyadondo Mashariki, nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu 'Bobi Wine' amepata matatizo ya figo na inaelekea kutokufanya kazi. 

Hii ni kwa mujibu wa Mawakili wake waliokwenda kumtembelea Mbuge huyo katika Kambi ya Jeshi ya Makindye anakoshikiliwa 

Kwa mujibu wa gazeti la Uganda la Daily Monitor, Madaktari hao hii leo kupitia Chama cha Madaktari nchini humo, (UMA), wako tayari kumpatia Mbunge huyo matibabu ya kitaalam ya hali ya juu ambaye sasa inaelezwa anapigania maisha yake katika kambi hiyo ya kijeshi 

Madkatari hao wametoa ombi hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mawakili wa Bobi Wine, wakisema mteja wao anahitaj haraka matibabu ya kitaalam ili kuokoa maisha yake. 

Hata hivyo wamesema hawawezi kutekeleza matibabu hayo bila kupata idhini kutoka Serikalini, kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Rais wa UMA, Dk. Ekwaro Obuku. 

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu dereva wa Bobi Wine, kuuawa kwa kupigwa risasi katika vurugu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arua . 

Staa wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amemuandikia barua ya wazi Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni kwa lengo la kumuombea msamaha msanii mwenzake huyo ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi hadi hivi sasa kwa tuhuma za uchochezi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad